Nina watoto 6 nje ya ndoa lakini bado mke wangu ananipenda sana, ninaogopa! - 2Baba Idibia

Msanii huyo mwezi Agosti mwaka jana alipata mtoto wake wa nane, sita wakiwa ni wale amezaa nje ya ndoa na wanawake tofauti huku wawili wakiwa wale amezaa na mkewe Annie.

Muhtasari

• Mapema 2baba akitoa kauli ya kuchukiza kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa wanaume wote wameumbwa tu kuchepuka.

• 2Baba ni baba wa watoto 8, wawili pekee wakiwa wale amezaa na Annie mkewe na wengine sita akiwa amewazaa na wanawake wengine.

2Baba na mkewe Annie
2Baba na mkewe Annie
Image: Instagram

Msanii wa Nigeria na baba wa watoto wengi, Innocent Idibia, anayejulikana kama 2Baba, amekiri wazi kwamba upendo wa mke wake Annie kwake unaweza kutisha wakati mwingine.

Baba huyo wa watoto saba alieleza haya katika nukuu za kipindi cha ukweli cha TV “Young, Famous, and African Reality Show,” kinachoendelea hivi sasa mtandaoni.

2Baba, katika mazungumzo na mwanahabari maarufu wa Afrika Kusini, Khanyi Mbau, alikiri waziwazi kwamba mkewe, Annie, anamwonyesha upendo zaidi kuliko yeye anavyodhani, na mapenzi yake wakati mwingine humtia wasiwasi sana kwani licha ya kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa na wakawake tofauti mara kadhaa, lakini bado anazidisha mapenzi kwake.

Khanyi alikuwa amemuuliza 2Baba, “Je, unajua jinsi anavyokupenda? Atajichoma ili kukuweka joto."

Akijibu, Mkali huyo wa kibao ‘African Queen’ alisema,

“Nafikiri nina….nadhani. Unajua…Ninahisi. Ndio, nahisi. Inatisha wakati mwingine. Siku zote amekuwa akinionyesha jinsi anavyonipenda. Anaionyesha zaidi kuliko mimi….. natambua ni wapi nimefanya makosa.”

"Ninatambua wapi ninapaswa kuongeza mchezo wangu. Wakati mwingine, mimi bado ni mlegevu lakini zaidi ya hayo yote, bado inategemea wewe kama mtu mzima. Ukweli ni kwamba, kuna baadhi ya mambo ambayo siwezi kurekebisha. Kiwango cha mwisho cha furaha hakitegemei mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe,” Aliongeza.

Awali, 2baba alikashifiwa vikali baada ya kutoa kauli ya kuashiria kutetea vitendo vyake vya kuzaa nje ya ndoa akisema kuwa ni mapungufu ya kila mwanaume kuchepuka na wanaume wote wameumbwa kutoka nje ya ndoa zao tu ili kujiridhisha.