Nyekundu aliyoonyeshwa Vinicius Jr baada ya 'kunyongwa' koo imebatilishwa

Mchezaji huyo alionyeshwa nyekundu licha ya kuwa yeye ndio alionekana kunyongwa, tukio ambalo lilizua malalamishi kutoka kwa mashabiki.

Muhtasari

• Winga huyo wa Brazil alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika za lala salama na mwamuzi  kwa kumpiga mpinzani kufuatia kuzozana.

Vinicius Jr alidondokwa na chozi baada ya kuoneshwa nyekundu licha ya kufanyiwa unyama uwanjani.
Vinicius Jr alidondokwa na chozi baada ya kuoneshwa nyekundu licha ya kufanyiwa unyama uwanjani.
Image: twitter

Kadi nyekundu ya mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr kwenye mechi ya Jumapili ya LaLiga huko Valencia, wakati pia alidhalilishwa kwa ubaguzi wa rangi, imefutwa, Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) lilisema Jumanne.

Winga huyo wa Brazil alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika za lala salama na mwamuzi Ricardo de Burgos Bengoetxea kwa kumpiga mpinzani kufuatia kuzozana na wachezaji wa Valencia ambapo Vinicius alionekana kushikwa shingoni.

Vinicius awali alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki kwenye Uwanja wa Mestalla, jambo lililopelekea mchezo huo kusimama kwa dakika 10 huku mchezaji huyo akionyesha watu waliokuwa wakimdhulumu uwanjani.

“Kamati ya Mashindano ya RFEF inaona kuwa tathmini ya mwamuzi iliamuliwa na kuachwa kwa uchezaji wote uliotokea, jambo ambalo liliathiri uamuzi wa mwamuzi,” shirikisho hilo lilisema.

"Ukweli kwamba yeye (mwamuzi) alinyimwa sehemu muhimu ya ukweli ilimfanya apitishe uamuzi wa kiholela. Na hii ni kwa sababu haikuwezekana kwake kutathmini vizuri kilichotokea."

Watu saba wanaotuhumiwa kwa uhalifu tofauti wa chuki dhidi ya Vinicius walizuiliwa na polisi wa Uhispania mapema Jumanne.

RFEF pia ilitangaza kuwa imeitoza klabu hiyo faini ya euro 45,000 ($49,536) na kwamba stendi ya kusini ya uwanja wa Valencia itafungwa kwa mechi tano.

Valencia waliita adhabu hiyo "isiyo na uwiano" na "isiyo ya haki", wakisema inadhuru mashabiki ambao hawakuhusika katika "tukio la aibu". Klabu hiyo iliongeza kuwa itakata rufaa ya kufungwa kwa sehemu ya uwanja huo.