Offset: Sina uhusiano wowote na Quavo na Marehemu TakeOff kutoka kundi la Migos

Kwa miaka migni, wengi walikuwa wanaamini kwamba watatu hao wana uhusiano wa damu haswa walivyokuwa na ukaribu katika kikundi cha Rap, Migos.

Muhtasari

• Offset alisema kuwa hapendi kabisa kuzungumzia kifo cha mwenzake TakeOff na muda mwingi hukaa katika hali ya kutoamini ili kuepuka fikira hizo.

• "Vitu vingine huwa siambii mtu yeyote. Hayuko hapa. Hiyo ni hisia ya uwongo, kaka," Offset alielezea baina ya majonzi.

Rapa Offset afichua kuwa hana uhusiano wowote wa damu na marehemu TakeOff wala Quavo kutoka kundi la Migos.
Rapa Offset afichua kuwa hana uhusiano wowote wa damu na marehemu TakeOff wala Quavo kutoka kundi la Migos.
Image: Instagram

Kwa miaka mingi, mashabiki waliamini kuwa wanachama wote 3 wa kundi la rap la Migos walikuwa na uhusiano, lakini Offset anaeleza ukweli ... akisema yeye hana uhusiano wowote na Quavo na Takeoff.

Kwa mujibu wa jarida la TMZ, Offset hivi majuzi aliketi kwa mahojiano mapya na Variety, ambapo alithibitisha kuwa Quavo ni mjomba wa Takeoff ... lakini dhana iliyoaminika kwa muda mrefu kuwa Offset ni binamu ya Quavo sio kweli.

Bado, Offset ana uhusiano mkubwa na Quavo na Takeoff ... Offset alikuwa mwanafunzi mwenzake wa Quavo walipokuwa wakikua huko Georgia, huku Offset akijumuika na Quavo na Takeoff wakati Offset alipokuwa darasa la sita. Wote wakawa wakubwa na hatimaye wakaunda kundi la muziki wa Rap la Migos.

Katika mahojiano ya Variety, Offset anasimulia kuhusu kolabo yake ya mwisho na Takeoff na tattoo yake mpya ya nyuma akimheshimu marehemu mwenzake, lakini alipata hisia alipoulizwa kuhusu kifo cha Takeoff na kunyamaza.

"Ni vigumu kwangu kuzungumza kuhusu s**t sasa hivi. Sijawahi kuzungumza kuhusu mambo haya," Offset alishiriki. "Kweli. Kuzungumza juu ya TakeOff ni ngumu, jamani. Kuzungumza juu ya haya yote ni ngumu. Ndio maana sisemi, kusema ukweli. Hiyo sh** inaumiza. Kama, itaniweka kwenye mhemko, na Sitaki kuwa katika hali hiyo."

"Vitu vingine huwa siambii mtu yeyote. Hayuko hapa. Hiyo ni hisia ya uwongo, kaka," Offset aliendelea, akielezea kuwa katika hali ya kutoamini kidogo ndivyo anavyoweza kuvumilia. "Ninapitia siku yangu nikifikiria kuwa ni bandia. Na sisemi chochote kwa mtu yeyote kuihusu."

Takeoff -- ambaye jina lake halisi lilikuwa Kirshnik Khari Ball -- alipigwa risasi na kuuawa huko Houston, Texas, Novemba 1, 2022. Alikuwa na umri wa miaka 28.