Otile akutana na mrembo 'kienyeji' mwenye tattoo zake, wafurahia chakula ghali pamoja

Otile Brown alikuwa ametoa ahadi ya kukutana na mrembo huo pindi baada ya kurejea nchini kutoka London.

Muhtasari

• Alhamisi jioni msanii huyo alikutana na mrembo huyo na kuelekea kwenye kwenye mgahawa wa kifahari ambapo walipata kusherehekea chakula cha jioni.

Otile Brown hatimaye akutana na kienyeji mrembo aliyechora tattoo zake.
Otile Brown hatimaye akutana na kienyeji mrembo aliyechora tattoo zake.
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya humu nchini Otile Brown hatimaye ametimiza ahadi yake kwa shabiki wake aliyechora tattoo zake mwilini mwake kama njia moja ya kuonesha jinsi anavyomkubali kimuziki.

Awali Otile alipokuwa ziara ya muziki nchini Uingereza, shabiki huyo alifanya mahojiano na chaneli ya Mungai Eve na kufichua kwamba aliamua kujichora tattoo za msanii huyo kwa sababu na mapenzi yake kwake.

Mrembo huyo kwa jina Kach alisema hata hivyo uamuzi wa kuchora tattoo za Otile haukupokelewa kwa njia chanya na marafiki zake kwani wengi walimdhihaki wakisema kuwa alikuwa anaharibu muda wake na Otile hangemtambua achia mbali kukutana naye.

Lakini kwa mshangao wa wengi, Otile aliona video ile na kutoa ahadi ya kukutana na mrembo huyo pindi baada ya kurejea nchini na pia kushiriki chakula cha jioni naye.

Alhamisi jioni msanii huyo alikutana na mrembo huyo na kuelekea kwenye kwenye mgahawa wa kifahari ambapo walipata kusherehekea chakula cha jioni.

Otile alipakia picha na video za tukio hilo adimu kwa mrembo huyo kienyeji kwenye instastories zake na wengi walimpongeza kwa kutimiza ahadi yake lakini pia ndoto ya mrembo huyo ya kutaka kukutana naye.

“Wengine walinitusi, waliniambia Otile Brown hawezi taka kienyeji kama wewe, Otile hatakutafuta, unaharibu tu muda wako bure, nikasema tu ni sawa,” Kach alisema kwenye video hiyo ambayo ilimvutia Otile wiki mbili zilizopita.

 “Waambie sijali Kach, wewe ni mtu wa ajabu sana na ninakubali upendo wako kwangu. Kienyeji huwa chenyewe. Kusema kweli nikija tutakuwa na mtoko wa chakula cha jioni na si kukutana kwa kahawa tu,” Brown alisema.