'Muache propaganda'- stanley omondi

Alimmiminia sifa Kennar na kusema kuwa Kennar ni Muundaji wa maudhui bora Zaidi Kenya.

Muhtasari

• Kumekua na uvumi baada ya stanley na Useful Idioty kutoonekana katika video za Crazy Kennar.

• Aliongeza kuwa hatakubali watu wamuaribia sifa muigizaji maafuru Crazy Kennar na kuwasihi wafuasi wake kuendelea kuziona video za Kennar na kumuonyesha upendo.

Waigizaji Crazy Kennar na Stanley Omondi.
Waigizaji Crazy Kennar na Stanley Omondi.
Image: INSTAGRAM

Muigizaji wa shoo ya Crazy Kennar Stanley Omondi amejitokeza na kusema kuwa Kennedy Odhiambo almaarufu Kennar hakumfukuza ila ni yeye aliyejiondolea ili kufanya video zake peke yake.

Ijumaa Stanley katika akaunti yake ya Twitter aliwakashifu watu wanaosema kuwa Kennar alimfukuza kutoka timu hio ya video vya uchekeshaji.

Alisisitiza kuwa Kennar hakumfukuza yeye na useful Idioty, waliokua wakiigiza katika video vya Crazy Kennar ila ni wao kwa makubaliano na mjasiriamali huyo waliojiondoa.

“Mimi na @crazy_kennar tuko vizuri tuache propaganda zinazoendelea. Kwa sasa siko kwenye skrini kwa sababu niliamua kufanya video zangu mwenyewe na ninafurahi zaidi kuwaona nyote mnazipenda,” aliandika Stanley.

Alifutilia mbali uvumi uliokua ukienea kuwa kennar aliwatimua wanaume na kuendelea kufanya video zake na wanawake pekee yake.

Kumekua na uvumi baada ya stanley na Useful Idioty kutoonekana katika video za Crazy Kennar.

Aliongeza kuwa hatakubali watu wamuaribia sifa muigizaji maafuru Crazy Kennar na kuwasihi wafuasi wake kuendelea kuziona video za Kennar na kumuonyesha upendo.

Alimmiminia sifa Kennar na kusema kuwa Kennar ni Muundaji wa maudhui bora Zaidi Kenya.

“mimi mtu akieza niulize niseme nani ‘content creator’ mzuri Zaidi kwa hakika kwangu ni Crazy Kennar, na nina uhakika ya kuwa chochote watu watasemaa kibaya kumhusu bado ataendelea kutengeneza video bora Zaidi.”