Wachaneni na pombe-Ujumbe wa Sandra Dacha kwa wasanii wenzake

Kulingana na hotuba yake Sandra Dacha aliwasihi wasanii hao kuacha tu kutumia pombe.

Muhtasari
  • Aidha mwigizaji huyo alisema kwamba kunywa pombe sio mbaya kwa starehe lakini wasivuke mipaka na kubuguia vileo kupita kiasi.
Sandra Dacha
Sandra Dacha
Image: Moses Mwangi

Mwigizaji Sandra Dacha ametuma ombi la unyenyekevu kwa wasanii kuwaambia wajiepushe na pombe.

Mtayarishaji wa maudhui alikuwa akizungumza wakati tasnia ya ubunifu ilikuwa ikitoa heshima kwa mcheshi marehemu Ochonjo.

Kulingana na hotuba yake Sandra Dacha aliwasihi wasanii hao kuacha tu kutumia pombe.

Aliendelea kusema kwamba, ikiwa daktari atakuambia uachane na pombe fanya tu. Kisha akasema kwamba, ikiwa daktari atakuambia uachane na nyama basi kula mboga.

Sandra alisema kuwawasanii wanapswa kutumia kile daktari amewashauri watumie hadi pale atakapowapa idhini ya kutumia kitu ambacho aliwanyima.

Aidha mwigizaji huyo alisema kwamba kunywa pombe sio mbaya kwa starehe lakini wasivuke mipaka na kubuguia vileo kupita kiasi.

"Wasanii, daktari akikwambia uache pombe, acha akikuambia uachane na nyama basi kula mboga hadi pale atakuambia tumia kitu hicho tena,huu ni wimbo tunaimba kama Diamond. Usinywe pombe ili kulewa," Dacha alieleza.

Dacha alisema walipompeleka Ochonjo hospitalini, waligundua kuwa alikuwa na hitilafu kwenye viungo kadhaa vya mwili wake na ilisikitisha kwamba hakuweza kupata usaidizi hospitalini.

"Kiambu imepauka, hakuna aliyemtunza Ochonjo. Alifariki tu," Dacha alisema.

Mwigizaji wa Ramogi TV Nyarkochia alishiriki maelezo ya mazishi ya mwigizaji Ochonjo na mashabiki wake huku akiomba maombi.

Nyarkoachia, alipokuwa akitoa taarifa kuhusu mipango ya mazishi, alishiriki ujumbe mzito, akiwatia moyo mashabiki kuhudhuria mazishi hayo.

Matamshi yake Sandra yanajiri siku chache baada ya mtangazaji wa Radiojambo Gidi kuwashauri wasanii wawekeze n wasitumie pesa zao kwa pombe na wanawake.

Gidi alitoa ushauri huo alip[okuwa ana mpongeza rappa maarufu Khaligraph Jones kwa maendeleo.