Wakisii, Wakikuyu na Wajaluo wajitokeza kwa wingi shoo ya Harmonize Texas, USA

Msanii huyo alionesha furaha yake baada ya mashabiki wake wa Kenya kujitokeza kwa wingi katika shoo yake huko Dallas, Texas.

Muhtasari

• Kwa furaha, Harmonize aliwatania Wakenya hao akisema kuwa alifurahia kuona wengi warembo wakiwa na makalio ya kupendeza.

Harmonize atoa shout outs kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi shoo ya Texas USA.
Harmonize atoa shout outs kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi shoo ya Texas USA.
Image: Instagram

Msanii Harmonize yuko nchini Marekani kwa ziara yake ya muziki kwa jina ‘Single Boy World Tour’ ambapo usiku wa kuamkia Jumamosi alikuwa katika jimbo la Texas.

Msanii huyo alifurahia idadi kubwa ya mashabiki wake kutoka Kenya ambao walijitokeza kwa wingi kupamba na kuipa shoo yake uhai, ambapo imekuwa ni vigumu sana katika siku za hivi karibuni kwa wasanii kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kupata mapokezi ya kisupastaa kwenye taifa hilo la wazungu.

Kwa Harmonize, mapokezi yalikuwa ya kishujaa, shukrani kwa mashabiki wake wa Kenya wanaoishi kwenye jimbo la Dallas, Texas.

Harmonize hakuwa mchoyo wa fadhila ambapo kupitia mitandao yake ya kijamii aliachia komenti za kishari na kiutani akiwatania mashabiki wake wa Kenya na hata kuwataja kwa makabila yao.

Miongoni mwa idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kwenye shoo yake, Harmonize aligundua kwamba Wakikuyu, Wakisii na Wajaluo walijitokeza kwa wingi na hata kuipamba kwa manukato ghali shoo yake, na hivyo asingemaliza siku bila kuwapa kile waingereza wanasema, Shout outs.

“Heshimu utandawazi,” Harmonize aliandika huku akiweka emoji ya kupiga saluti kwa Wakikuyu ambao aliwatania kwamba kwenye hiyo shoo alipata ukweli kinyume na dhana ambayo inadai kwamba warembo wa kabila hilo huwa hawana makalio.

Harmonize MAREKANI
Harmonize MAREKANI

Pia msanii huyo alitoa shukrani kwa Wajaluo na Wakisii akisema kuwa waliifanya shoo yake kuwa ya kipekee na ya kukumbukwa.

“Luo na Kisii mmefanya maisha yetu kuwa mseto sana. Mlitesa sana,” Harmonize aliandika kwenye instastory yake.

Hata hivyo, akiwa na furaha nyingi, Harmonize aliandika kwamba si yeye alikuwa anaandika bali ni mwanadada wa Kikuyu ambaye alichukua simu yake na ndiye alikuwa anaandika maneno hayo.