Nitamwambia nini binti yangu siku ya kina baba duniani? - Mkewe AKA azidiwa na hisia

Mrembo huyo alisema kuwa kila mara hupata ukakasi mwingi anaposikia watu wakimtajia Durban, jiji alikouliwa AKA.

Muhtasari

• Zinhle alieleza kwa majonzi kwamba kwa muda mrefu binti yake alikuwa anamsherehekea baba yake siku ya kina baba duniani.

Mke wa AKA ni mwenye mawazo mengi kuhusu kile atamwambia binti yake siku ya kina baba dunaini.
Mke wa AKA ni mwenye mawazo mengi kuhusu kile atamwambia binti yake siku ya kina baba dunaini.
Image: Instagram

Huku ulimwengu ukijiandaa kusherehekea siku ya kina baba kote duniani mwezi kesho tarehe 18, kwa DJ Zinhle ambaye ni mke wa rapa marehemu AKA aliyeuawa mwezi Februari nchini Afrika Kusini hali si ya wasiwasi.

DJ Zinhle katika mahojiano yake ya kwanza na wanahabari takribani miezi mitatu tangu kifo cha ghafla cha baba wa mtoto wake Kairo Forbes, alionyesha wasiwasi wake mkuu kuhusu ni maelezo gani atampa binti yake Kairo ikifika siku hiyo ya kusherehekea kina baba.

Zinhle alieleza kwa majonzi kwamba kwa muda mrefu binti yake alikuwa anamsherehekea baba yake kwa kushirikiana naye ifikapo siku ya kina baba duniani, kila mwaka mwezi Juni, lakini mwaka huu mambo kidogo yatakuwa mazito kwake kwajni hajui atamweleza nini kuhusu kilichomtokea baba yake.

“Ni nini nitakwenda kumwambia binti yangu kuhusu baba yake ikifika siku ya kina baba duniani?” Zinhle alijiuliza kwa majonzi mbele ya wanahabari.

Kila mtu anajua Kairo na AKA walikuwa na uhusiano mzuri. Wawili hao kila mara walikuwa na hisia zao kwa video zao nzuri za densi na wakati wa baba-binti, haswa Siku ya Akina Baba.

Awali, mcheza santuri huyo aliweka wazi kuwa kila mara anaposikia mtu akimtajia jina la jiji la Durban huingiwa na kiwewe na woga kwani huko ndiko baba mtoto wake alikouawa mwezi Februari.

Alisema kuwa hayuko tayari kifikira na kihisia kwenda Durban licha ya kualikwa katika kuwa mmoja wa watumbuizaji wa hafla moja ya kimuziki huko Durban itakayofanyika mwezi Julai.

“Siwezi kuwadanganya, siko tayari kwenda Durban. Kihisia, siko tayari hata kidogo. Ninapata wasiwasi kidogo kuhusu kuwa Durban. Itachukua muda kabla ya kuwa Durban."