logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watalaka pande moja: Ex wa Hakimi amfariji Shakira kwa kuachwa na Gerald Pique

Shakira waliachana na Pique miezi michache iliyopita kabla ya Hiba pia kuachana na Hakimi.

image
na Radio Jambo

Makala30 May 2023 - 11:36

Muhtasari


• Kwa kuzingatia changamoto zake binafsi, mwigizaji huyo wa Kihispania alishiriki wimbo wa Shakira "Acrostico"

• Wimbo huo ulikuwa umeambatanishwa na ujumbe mzito unaosisitiza umuhimu wa familia, ambayo inapaswa kuja ya kwanza mbele ya kila kitu.

Mtalaka wa Hakimi asimama na mtalaka wa Pique

Hiba Abouk, mpenzi wa zamani wa beki wa pembeni wa Paris Saint-Germain Achraf Hakimi, alionyesha mshikamano wake na Shakira kwa kumtumia ujumbe kupitia mitandao ya kijamii, jarida la Marca liliripoti.

Abouk amekuwa akishughulikia maswala ya kibinafsi yanayohusiana na Hakimi katika wiki za hivi karibuni, kufuatia habari za madai yake ya kumpiga mwanamke mwenye umri wa miaka 24.

Wakati huu, Abouk amepata faraja kwa watoto wake wawili wadogo, Amin na Naim. Kwa kuzingatia changamoto zake binafsi, mwigizaji huyo wa Kihispania alishiriki wimbo wa Shakira "Acrostico" pamoja na ujumbe mzito unaosisitiza umuhimu wa familia, ambayo inapaswa kuja ya kwanza mbele ya kila kitu.

"Kuwa mvumilivu sana kwako mwenyewe," aliandika.

“Endelea kujikumbusha kuwa mambo yanakuendea. Jambo ambalo halina maana sasa hivi karibuni litakupa amani na uwazi. Utaelewa kwa nini mambo fulani hutokea kwa njia fulani. Yote ni kwa wakati wa kimungu. Kaa chanya,” Abouk aliandika kama ilivyoripotiwa na jarida hilo la Kihispania.

Pique na Shakira walitengana miezi michache iliyopita na mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona amekuwa akionekana kupiga misele mitaani na mwanadada mrembo ambaye aliweka wazi kuwa ni mbadala wa Shakira.

Kwa upande wake, msanii huyo kutoka Colombia baada ya kutalikiana na Pique akielekea zake Miami Marekani kuishi na watoto wake waili katika kile alisema kuwa hangetaka kuwahusisha katika sakata zima la kuchafuana na baba yao wakiwa nchini Uhispania.

 

Abouk amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii katika wiki za hivi karibuni, huku wengine wakimtuhumu kwa kutafuta sehemu ya mali ya mwanasoka huyo wa Morocco. Hata hivyo, anabakia kuzingatia kutanguliza ustawi wa watoto wake wawili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved