logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jovial akumbuka kifo cha babake kutokana na saratani ya ubongo

Mwimbaji Jovial  amemkumbuka babake aliyeaga kutokana na saratani ya ubongo.

image
na

Michezo06 June 2023 - 10:41

Muhtasari


• Mwimbaji huyo alisema kuwa kumbukumbu ya babake ililetwa na kurekodi kwa wimbo wake mpya, Don’t Give Up uliowafanya kila mtu aliyehusika kutokwa na machozi.

• Jovial aliendelea kueleza jinsi ilivyokuwa uchungu kwake kumtazama baba yake akikata roho bila kuwa na uwezo wa kumsaidia.

Jovial

Mwimbaji maarufu Jovial  amemkumbuka marehemu babake ambaye aliaga baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

Mwimbaji huyo alisema kuwa kumbukumbu ya babake ililetwa na kurekodi kwa wimbo wake mpya, Don’t Give Up akimshirikisha Lexsil ambao uliwafanya kila mtu aliyehusika kutokwa na machozi.

"Kurekodiwa kwa wimbo wa 'dontgiveup' ulikuwa mgumu, tulilia sana. kila mtu alikuwa na hadithi zake za kibinafsi na iliniumiza sana. Nilimpoteza baba yangu kwa saratani ya ubongo, jambo ambalo liliniuma sana, hata hadi leo nikikumbuka natokwa na machozi . Kuna siku mimi hukumbuka baba alishimdwa kumtambua mtu yeyote na hata mimi mtoto wake hakuweza kuongea nilipotaka aongee nami, ” alikumbuka.

Jovial aliendelea kueleza jinsi ilivyokuwa uchungu kwake kumtazama baba yake akikata roho bila kuwa na uwezo wa kumsaidia.

"Kwangu alikuwa shujaa wangu lakini niliona shujaa wangu akifa na hakuna kitu ambacho ningefanya . Ninapotazama video ya wimbo wangu kama kila mtu mwingine natokwa na machozi na kujazwa na huzuni tele,"aliongeza.

Jovial pia aliwatia moyo mashabiki wake na kuwaambia kuwa ata wakikabiliwa na tatizo lolote wasikate tamaa.

"Naomba wimbo huu uzungumze na mtu, tafadhali pigana, pigana kila siku. Usichoke kupigana, piga magoti, pigana ata kama ni kiafya. Sio lazima hadithi ya kila mtu iwe sawa, "aliongeza.

Wimbo huo pia uliwashirikisha mwigizaji wa zamani wa Machachari, Tyler Mbaya almaarufu Baha na mpenzi wake Georgina Njenga.

Hadithi ya Baha inalandana na ile ya Jovial kwani mwaka wa 2013 mwigizaji huyo alimpoteza mama yake kwa ugonjwa wa saratani.

Wapenzi hawa wawili hivi majuzi walikua wameibua uvumi kuwa hawakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tena hii ni baada ya kuacha kufuatiliana katika mtandao wa Instagram.

Aidha baada ya wimbo wa Jovial kutolewa Wakenya wangu walihisi hii ilikuwa njia moja ya kutafutia wimbo huo umaarufu na madai ya Bahati kuachana na Georgina ulikuwa kiki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved