Mcheshi Mwalimu Rachel ameelezea kujutia kusimamia kundi maarufu la muziki wa Gengetone, Sailors.
Katika video aliyopakia kwenye akaunti yake ya Instagram Mwalimu Rachel alisema kusimamia Sailors ulikuwa uamuzi wa kujutia maishani hadi sasa.
Katika mahojiano hayo Mwalimu Rachel alifichua sababu ya kutengana na kundi hilo ilikuwa kwa ya kutoelewana na wanachama.
Mwalimu Rachael alishutumiwa na wafuasi wa kundi hilo kwa kunyakuwa akaunti ya YouTube ya Sailor.
Kutokana na dhana ya wafuasi wa Sailors, mtangazaji huyo alikiri kuwa yeye na mwanawe walipokea vitisho vya kuuawa mtandaoni.
“Vitisho ambavyo nimekumbana navyo mtandaoni imenitikisa sana. Mimi na mwanangu tumepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa mashabiki kwa sababu ya chaneli hiyo ya YouTube,” alisema Mwalimu Rachael.
Mwalimu Racheal alikemewa kwa madai ya kuwa kizuizi kwa taaluma ya wanamziki hao, tuhuma ambazo alipinga vikali.
"Sikuua taaluma yao. Huenda watu wanafikiria nilifanya hivyo, na wamefikia hatua ya kuwataka mabosi wangu wanifukuze kazi, licha ya kutojua lolote kuhusu kisa cha kweli.”
Kikundi hicho cha muziki kilijumuisha Peter Miracle Baby, Shalkido, Cocos Juma, Masilver na Lexxy Yung.
Kundi hilo lilipata umaarufu na wimbo wao Wamblambez mwaka wa 2018 wakati mtindo wa Gengetone ulivuma kote nchini ya Afrika Mashariki.