Jinsi msanii Rema alivyopata 'six pack' bila kunyanyua vyuma vya mazoezi kwenye gym

"Nilipokuwa Ghana nilipokuwa nikihangaika, nikifanya kazi ngumu. Tayari nilikuwa nikivurugwa kutoka kwa chochote nilichokuwa nikifanya." - Rema.

Muhtasari

• Alieleza jinsi, wakati yeye na familia yake walipokuwa wakiishi katika Jiji la Benin, jimbo la Edo, alikuwa akibeba ndoo za maji.

Msanii Rema asimulia jinsi alivyopata six pack bila kwenda gym.
Msanii Rema asimulia jinsi alivyopata six pack bila kwenda gym.
Image: Instagram

Msanii kinda kutoka Nigeria ambaye anazidi kutamba na kibao cha ‘Calm Down’Rema amekiri, kwa njia ya kuchekesha jinsi alivyopata mapande sita almaarufu six pack kwenye mwili wake.

Kwa kawaida, watu wenye misuli iliyotuna na kutitimuka wanadhaniwa kuwa wale wanaojibidiisha kwenye mazoezi kwenye gym, lakini kwake Rema, si hivyo.

Msanii huyo katika mahojiano kwenye mtandao wa Spotify, alisema kwamba hakufanya kazi ya kunyanyua vyuma kwenye gym ili kupata ‘six pack’ za kushangaza, sifa ya utu wake ambayo inawafanya wafuasi wake wa kike kubweteka, lakini badala yake misuli yake ilijitokeza tu na kutuna kutokana na kufanya kazi ngumu za sulubu.

Mwanamuziki huyo alifichua hayo katika mahojiano na mtandao wa Spotify, na kuongeza kuwa kufanya kazi kwa bidii na fani za malipo ya chini kulimsaidia kujenga mwili wake.

Alieleza jinsi, wakati yeye na familia yake walipokuwa wakiishi katika Jiji la Benin, jimbo la Edo, alikuwa akibeba ndoo za maji. Rema anadai kuwa aliendelea kuhangaika na kukua zaidi wakati alipokuwa Ghana.

Alisema; "Siendi kwenye mazoezi. Siku zote nilikuwa na mifumo ya mwili wangu, huko nyuma tangu Benin, nikichota maji, nikibeba ndoo za maji, unajua, mikokoteni.”

"Nilipokuwa Ghana nilipokuwa nikihangaika, nikifanya kazi ngumu. Tayari nilikuwa nikivurugwa kutoka kwa chochote nilichokuwa nikifanya. Unajua, siku ambazo nilikuwa na njaa, mapande yanug sita yaitokea tu bila shinikizo [vicheko].”

Msanii huyo amekuwa wa kwanza kuandikisha na kuvunja rekodi za takwimu za streams kwenye majukwaa ya kupakua miziki, huku remix ya Calm Down aliyomshirikisha Selena Gomez ikiendelea kuvuruga kwenye chati za Billboard kwa Zaidi ya mwezi sasa.