"Nitaambia nini maadui zangu" Uamuzi wa CS Namwamba wamliza Akothee

"Nitawaambia nini maadui zangu na vile nilikuwa nawataarifu kila kitu kuhusu mafanikio yangu? Suti nimeshona juzi na hata sijavaa, halafu kazi imeisha..." - Akothee alilia.

Muhtasari

β€’ Waziri wa vijana na michezo Ababu Namwamba alikuwa amewateua watu maarufu akiwemo Akothee mwezi Fenruari kwenye baraza la Talanta Hela lakini Ijumaa alibatilisha uteuzi wao.

Akothee alia kusimamishwa kazi Talanta Hela,
Akothee alia kusimamishwa kazi Talanta Hela,
Image: Instagram

Msanii na mjasiriamali Akothee ameonesha mshangao na kutoridhishwa kwake na uamuzi wa waziri wa michezo na maswala ya vijana Ababu Namwamba kuvunja baraza la Talanta Hela, miezi michache baada ya kuteuliwa kwake.

Mwezi Februari, Waziri Namwamba aliwateua watu maarufu kadhaa wa humu nchini akiwemo Azziad Nasenya, Akothee, Churchill, Kate Actress, Carol Radull miongoni mwa wengine katika baraza la Talanta Hela.

Talanta Hela ilizinduliwa Ijumaa katika ikulu ya Nairobi lakini saa chache baadae waziri Namwamba kwenye vyombo vya habari alitangaza kubatilishwa kwa uteuzi wa maceleb hao.

Habari hizi zilimfikia kwa njia hasi msanii Akothee ambaye licha ya kusema alipata nafuu dhidi ya kusimangwa kwamba alikuwa anajivinjari na pesa ya walipa ushuru, lakini kwa upande mwingine alilia kuwa sasa ubatilishwaji wa uteuzi wake utawapa maadui zake nafasi kubwa ya kumsakama kwenye koo hata Zaidi.

β€œAii maadui zangu, aaai aai. Maadui zangu sasa watasherehekea. Wale ambao hawakuwa wanalala kwa sababu ya mafanikio yangu sasa watapata usingizi. Aai maadui zangu leo watapata sababu ya kulala na vile nilikuwa nimeanza kung’ara. Unaamkaje na kubatilisha uteuzi wangu hivyo tu? Na unajua niko na maadui ambao wanaangalia katika mafanikio yangu. Aaah! Nitaamkaje kwa habari mbaya kama hizi na jinsi mwaka ulianza vizuri kwangu? Na vile nilikuwa nawataarifu maadui zangu kila kitu kizuri kwangu, mbona wizara mbona?” Akothee alilia.

Hata hivyo, msanii huyo alijiliwaza kwamba kwa vile yeye hakutajwa, pengine bado kazi yake iko na wale waliotajwa pekee ndio pengine uteuzi wao ulibatilishwa.

β€œJe, nirudije na kuwaambia nini maadui zangu? AhhhhSaniambia mtu asikuje hapa nimeeenda honey moon na pesa za sirikali , ama nalisha Omondi na pesa ya Tax. Wasee tumefikiwa , Bora mimi sijatajwa , hao kwa list ndio hawana kazi mimi bado niko job, suti nimeshona juzi hata sijavaa,” Akothee alilia.