Msanii Akothee kupitia ukurasa wake wa Instagram ameendelea kumsherehekea mtoto wake wa kiume ambaye anamuita Mr Switzerland.
Msanii huyo alipakia picha za mtoto huyo ambaye anamuita Ojwang pia na kusema kuwa furaha yake kama mama ni pale anapomuona tabasamu lake, miguu yake mirefu na moyo wake, vyote ambavyo amechukua kutoka kwake.
Akothee alisema kuwa ana ndoto ya kumzalia mpenzi wake Omoshi mtoto, huku pia akijaribu kutafakari jinsi mtoto huyo atakavyokuwa.
Kulingana na mjasiriamali huyo, mtoto ambaye atamzalia mpenzi huyo wake ambaye wamefunga harusi mwezi Aprili atakuwa na muonekano wa kipekee, hii ikiwa na makalio madogo na mwili mwembamba.
Hata hivyo, Akothee alisema kuwa ana Imani hiyo licha ya kutojua ni kwa nini analazimika kuamini hivyo.
“MR SWITZERLAND. The long legs , his heart ,his smile are All mine.My first born Son.Ojwang π€£π€£ I have a feeling Omosh baby will have a small nyash ,and and a tiny body π€£π€£π€£π€£ I don't know why π€£π€£π€£ ππππ” Akothee alisema.
Msanii huyo hajaacha maneno ya watu kumkomesha au kumdunisha kwa jinsi anavyosherehekeka penzi lake na mpenzi wake Omoshi, huku wiki chache zilizopita wakienda fungate katika kisiwa cha Santorin nchini Ugiriki.
Akothee anasema kuwa aliolewa na rafiki wake wa karibu na hawezi subiri kumlazia mtoto hatimaye, mtoto ambaye tayari hata kabla ya kumzaa, ameshaanza kuona picha yake katika ulimwengu wa kifikira.