Guiness World Records watambua rekodi iliyowekwa na mpishi wa Nigeria, Hilda Baci

Rekodi ya marathon ndefu zaidi ya kupikia na mtu binafsi ilivunjwa na Baci mwezi wa Mei tarehe 15 baada ya kupika kwa saa 100.

Muhtasari

• Katika akaunti yake rasmi ya twitter Guiness World Records walisema kuwa baada ya kukagua ushahidi uliowasilishwa na Baci walirithika na sasa wamedhibitisha rekodi hiyo.

• Rekodi hiyo ilivunja rekodi iliyowekwa na mpishi kutoka India anayefahamika kwa jina Tata London.

Hilda Baci, mpishi wa Nigeria aliyepika kwa saa 100 mfululizo.
Hilda Baci, mpishi wa Nigeria aliyepika kwa saa 100 mfululizo.
Image: Instagram

Guiness World Records hatimaye imeweza kuitambua rekodi iliyovunjwa na mpishi Hilda Effong Bassey almaarufu Hilda Baci kutoka Nigeria ya kupika kwa muda mrefu zaidi.

Rekodi ya marathon ndefu zaidi ya kupikia na mtu binafsi ilivunjwa na Baci mwezi wa Mei tarehe 15 baada ya kupika kwa saa 100 ili kuweka Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa saa ndefu zaidi za kupikia na mtu binafsi.

Katika akaunti yake rasmi ya Twitter Guiness World Records walisema kuwa baada ya kukagua ushahidi uliowasilishwa na Baci walirithika na sasa wamedhibitisha rekodi hiyo.

"Baada ya kukagua video za upishi, tunafuraha kutangaza kuwa Hilda Baci ndiye mshikilizi wa rekodi ya marathon ya upishi,"

Hilda Baci alijawa na furaha baada ya rekodi hio kudhibitishwa na kuandika kwenye akaunti yake ya Twitter "Hii ni habari bora zaidi, asanteni sana."

Mpishi huyo mwenye umri wa miaka 26 alianza kupika Mei 11 na akaendelea na mapishi yake hadi tarehe 15 Mei, siku tano mfululizo akipika zaidi ya chakula aina 100.

Guiness alipunguza masaa ya mapishi hayo kutoka masaa 100 hadi masaa 93 baada ya Baci kuchukua mapumziko alipokuwa akianza kupika.

Rekodi hiyo ilivunja rekodi iliyowekwa na mpishi kutoka India anayefahamika kwa jina Tata London.

Tata alipika kwa muda wa masaa 87 na akika 45 mfululizo.

Mwezi Mei Guiness World Records ilisema kuwa bado haijatambua rekodi hiyo kwa kuwa hawakuwa wamepata ushahidi wa kupika kwa Hilda na walihitaji kuzipitia video hizo ili kuidhinisha rekodi hiyo.

"Tunafahamu kuhusu jaribio hili la ajabu la rekodi, tunahitaji kupitia ushahidi wote kwanza kabla ya kuthibitisha rasmi rekodi".

Mpishi Mkenya Mohammed Maliha alijitosa ulingoni na kusema kuwa anapania kulivunja rekodi hiyo ya Hilda Baci mwezi Agosti baada ya kutamatisha majaribio ya upishi tarehe 26 mwezi Mei.

Mpishi huyo anayeishi Mombasa amewai kuvunja rekodi hio ya Guinness Book of Records mara mbili.

Je,muda wako mwingi kutumia katika mapishi ni masaa mangapi?