Mmiliki wa jumba alikoishi AKA atoa notisi kwa familia kuondoa vitu vyake, kumbe halikuwa lake!

"Haikuwa nyumba yake. Alikuwa akikodisha nyumba hiyo na alikuwa akilipa kila mwezi. Najua watu walidhani hii ilikuwa nyumba yake kwa sababu ya magari aliyokuwa akiendesha."

Muhtasari

• Miongoni mwa magari yaliyokuwa yakiendeshwa na Supastaa huyo, ni BMW i8 yenye thamani ya angalau R2-milioni (Ksh 15m).

• Pia alimiliki BMW X7 yenye thamani ya zaidi ya R2.6-milioni (Ksh 19.6m) alizonunua muda mfupi kabla ya kifo chake.

Nyumba aliyokuwa akiishi AKA yawekwa sokoni na mwenye nyumba halisi licha ya wengi kudhani nyumba hiyo ilikuwa inamilikiwa na msanii huyo.
Nyumba aliyokuwa akiishi AKA yawekwa sokoni na mwenye nyumba halisi licha ya wengi kudhani nyumba hiyo ilikuwa inamilikiwa na msanii huyo.
Image: Screengrab

Siku mbili zilizopita, kuliibuka na taarifa zenye ukakasi kwamba mmiliki wa jumba alikokuwa anaishi msanii marehemu wa Afrika Kusini AKA ametoa notisi kwa familia yake kuondoa vitu vyote vya msanii huyo huku akitaka kulipiga mnada sokoni.

Taarifa hizi ziliwaacha wengi vinywa wazi, kwani walikuwa wanajua jumba hilo la kifahari lilikuwa la msanii huyo kumbe alikuwa tu mpangaji.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, AKA alikuwa analipia kodi ya randi za Afrika Kusini elfu 30 kwa kila mwezi sawa na shilingi laki mbili na elfu 25 za Kenya.

Jarida la Sunday World la nchini Afrika Kusini liliripoti kwamba mmiliki wa jumba hilo la kifahari alitoa notisi hiyo baada ya kukatisha mkataba wa AKA miezi michache tu baada ya kifo chake.

“Haikuwa nyumba yake. Alikuwa akikodisha nyumba hiyo na alikuwa akilipa takriban R40 000 kwa mwezi. Najua watu walidhani hii ilikuwa nyumba yake kwa sababu ya magari aliyokuwa akiendesha,” alisema mshirika wa karibu wa AKA, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa hofu ya kudhulumiwa, kulingana na jarida hio.

Miongoni mwa magari yaliyokuwa yakiendeshwa na Supastaa huyo, ni BMW i8 yenye thamani ya angalau R2-milioni (Ksh 15m) na BMW X7 yenye thamani ya zaidi ya R2.6-milioni (Ksh 19.6m) alizonunua muda mfupi kabla ya kifo chake.

Mshirika huyo alisema Mekoa, mmiliki wa jumba, aliiambia familia ya AKA kuwa alikuwa amekatisha makubaliano ya kukodisha na kuwataka waende kwenye jumba hilo na kuchukua mali yake.

"Walizikusanya na inaonekana kuzifungia kwenye hifadhi," mshirika huyo alisema.

Hii licha ya AKA, mzaliwa wa Kiernan Forbes, kudaiwa kulipa kodi yake mapema hadi Septemba mwaka huu.