Diamond Platnumz akiri kufunga ndoa kabla mwaka huu kukamilika

Msanii huyo alidokeza kwamba ikiwemo yeye atafunga ndoa na msanii wake Zuchu, baada ya msanii huyo kumpa zawadi ya maua siku ya kina baba duniani.

Muhtasari

• Diamond alisema hayo baada ya mmoja wa wafanyikazi wake wa Wasafi, Don Fumbwe kufunga ndoa wikendi iliyopita.

Diamond akiri kufunga ndoa mwaka huu
Diamond akiri kufunga ndoa mwaka huu
Image: Facebook

Msanii Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba azimio kuu la wafanyikazi wake wote ndani ya kampuni ya Wasafi kutoka kwa redio, runinga, lebo na Kamari, ambao hawajapata ndoa hadi sasa, ifikapo mwisho wa mwaka huu atahakikisha kila mmoja amepata ndoa.

Diamond aliandika haya kupitia instastories zake ambapo alipakia video fupi inayowaonyesha maharusi wa kiislamu wakishiriki nikkah.

Msanii huyo hata hivyo pia aliwatania mashabiki wake kuwa watawachosha kwa kuwaitisha michango kwani ni wanaume wengi sana ndani ya kampuni ya Wasafi ambao bado hawajapata ndoa.

“Mwaka huu kama Wasafi tumeamua wote tusiokuwa na ndoa kuoa, mjiandae kwa michango,” Diamond alisema.

Alibainisha kwa njia ya utani kwamba katika wafanyikazi hao wote wa familia ya Wasafi, kuna makundi matatu yakijumuisha wale ambao wataoa mwanamke mmoja, wengine wataoa wawili na wengine hadi watatu na wanne.

Msanii huyo alifichua kwamba walikuwa katka harusi ya mmoja wa wafanyikazi wake, Don Fumbwe ambaye anasimamia kitengo cha ulipaji mishahara kwa wafanyikazi.

“Kuna wanaooa mmoja, kuna wawili na watatu... ndugu yetu Don Fumbwe kafungua dimba,” Platnumz aliandika.

Ikumbukwe kwamba msanii huyo si mseja kwani amewahi jaribu guu lake katika dimba la ndoa si mara moja wala mbili na mahusiano yote yalisambaratika baada ya muda, yakimuacha akiwa na watoto na kina mama tofauti.

Msanii huyo alionesha dalili zote za kutulia alipochumbiana na mwanamitindo Hamisa Mobetto na walipopata mtoto mmoja baadae walaichana na Diamond hakusubiri moto kupoa, alijipata katika mahusiano mengine na mwanamitindo kutoka Uganda Zari Hassan ambaye walikaa naye kwa muda licha ya masimango kutoka kwa wengi kuwa alikuwa mkubwa kiumri kuliko msanii huyo mkurugenzi wa Wasafi.

Baada ya miaka kadhaa, waliachana wakiwa na watoto wawili na Diamond akajitosa kwenye mahusiano tena na aliyekuwa mtangazaji kutoka Kenya, Tanasha Donna. Pamoja walizaa mtoto mmoja na wakaachana na amekuwa akisemekana kuwa anatoka kimapenzi na Zuchu, msanii wake.