DJ Fatxo ambaye amekuwa kweney vichwa vya habari katika miezi minne iliyopita kwa sababu nyingi hasi, amefichua maisha yake kwenye mahusiano ambapo ameendelea kusisitiza kwamba yeye si shoga.
Fatxo amekiri kwamba ana mpenzi wake ambaye wamekuwa wakichumbiana kwa takribani miaka miwili sasa, lakini pia amefichua kwamba katika tasnia ya Sanaa, kama mtu mwingine yoyote yule, kuna mtu maarufu ambaye moyo wake hauachi kuongeza kasi ya mapigo pindi anapomuona, iwe uso kwa uso au mitandaoni.
Katika chaneli ya YouTube ya Obinna, Msanii huyo wa Mugithi aliulizwa swali kuhusu celeb ambaye anamkubali na kumpenda, kwa mshangao alimtaja msanii wa kizazi kipya Nadia Mukami akisema kuwa ni msichana mzuri, mpole na mrembo ambaye ni ndoto ya kila mwanamume.
Mwanzoni alisita kumtaja, akisema kuwa ni mke wa mtu lakini baada ya kushawishiwa, alimtaja na kujitetea kwamba ni kawaida kila mtu ako na yule celeb ambaye anampenda lakini hajawahi pata nafasi ya kumwambia.
“Yule ambaye nikimpata napita naye? Ni mke wa mtu acha nisiseme…Nadia, Nadia... Nadia Mukami. Ni msichana mpole na mrembo. Kusema kweli ako vizuri. Kila mtu hakosi celeb crush wake hata yeye ukimuuliza atasema ako na watu wake wenye anapenda,” Fatxo alisema.
Alisema kuwa pengine hata Nadia hamjui na hivyo ni vigumu sana kwake akiulizwa aseme ni Fatxo ndio anamfia.
Msanii huyo kwa mara nyingine tena alipata nafasi ya kuzungumzia chimbuko la kuhusishwa na ushoga akisema kuwa ni baadhi ya wanablogu wa Kirinyaga ambao walikuwa wamelipwa ili kujaribu kumchafulia jina kipindi cha sakata kuhusu kifo cha utata cha Jeff Mwathi.
“Walianikwa ao wajinga, si ni watu wa Kirinyaga weney walikuwa wanapanga huo ujinga. Ni kitu ilikuwa imepangwa. Angalia katika machapisho ya Obare, alionesha screenshots zote hadi wakinipangia hadi picha zangu zimewekwa hapo.. ni wanablogu ambao nafikiri hawakulipwa na watu Fulani wa Mwea. Yaani hadi wameandika vizuri hapo, acha tuite huyu jamaa shoga ndio tuweze kumshikanisha na yule jamaa wa Mwea… hata hiyo Mercedes yake acha tuseme alinunuliwa na huyo jamaa wa Mwea…” alisema.
Alisema kuwa huyo mtu wa Mwea ni mfanyibiashara ambaye alikuwa kama balozi wake wa mauzo ya mchele kitambo wakati anaanza kwenye tasnia ya burudani.
“Hii ilikuwa simulizi iliyokarabtiwa. Baada ya yote walichokuwa wakitaka ilikuwa ni kunifanya nichukiwe na watu,” alisema.