Msanii maarufu wa nyimbo za Bongo, Diamond Platnumz ametegua mtego wa meneja wake Baba Tale wa kumtaka aoe.
Mwanamuziki huyo na mmiliki wa radio ya Wasafi Fm alisema hawezi kumpiku bwana harusi, Don Fumbwe, labda tu aoe wanawake wawili licha ya ushauri wa meneja wake kumtaka Diamond kumpiku bwana harusi na kufunga ndoa hivi karibuni.
"Baba tale alisema nimpiku Don Fumbwe, lakini ili kumpiku labda nioe wake wawili, lakini mimi siezi mpiku itakuwa kumkosea heshima ndugu yangu."
Diamond alikiri kuwa yeye hakuwa mtaalamu wa maswala ya ndoa alipoalikwa kuwashauri wanandoa hao.
"Mimi katika swala la ndoa siezi kushauri kaka yangu, mimi kitu kimoja tu nitakushauri katika mahusiano si kila wakati uwe mshindi ukitaka kuishi na mtu, si kila argument wewe ndie uwe mshindi wakati mwingine ata kama umeshinda mwachie ashinde."
Ikumbukwe kwamba msanii huyo si mseja kwani amewahi jaribu guu lake katika dimba la ndoa si mara moja wala mbili na mahusiano yote yalisambaratika baada ya muda, yakimuacha akiwa na watoto na kina mama tofauti.
Diamond akizungumza katika harusi hiyo aidha alizungumzia umuhimu wa uaminifu katika biashara na maisha kwa jumla lakini alisistizia umuhimu wa uaminifu katika mahusiano ya kimapenzi.
"Kikubwa bila uaminifu ni vigumu sana kufanikiwa bila kuwa mwaminifu, si kwenye fedha tu bali katika mahusiano ya kimapenzi."
Meneja wake Diamond, Babu Tale alimshauri Diamond afanye harusi na kuwaongoza wasanii na wafanyikazi wa kampuni ya Wasafi kutoka kwa redio, runinga, lebo na Kamari katika safari ya kufunga ndoa.
"Umpiku Makame, umfunike Makeme,uoe utuonyeshe na sisi kuwa wewe unaoa."
Jumatatu,Diamond Platnumz aliweka wazi kwamba azimio kuu la wafanyikazi wake wote ndani ya kampuni ya Wasafi ambao hawajapata ndoa hadi sasa, ifikapo mwisho wa mwaka huu atahakikisha kila mmoja amepata ndoa.