Video: Nabii apata ufunuo wa Mungu kumtaka Davido kuuza gari alilonunua Mei

Davido alinunua gari hilo aina ya Maybach Virgil Abloh la 2023 ambalo alilinunua kwa thamani ya shilingi milioni 110. Kampuni hiyo ilitengeneza magari 150 pekee.

Muhtasari

• Mwezi mmoja uliopita, iliripotiwa kwamba msanii Davido alijinunulia gari la kifahari aina ya Maybach Virgil Abloh la 2023.

Nabii apata ufunuo wa kumtaka Davido kuuza hari lake.
Nabii apata ufunuo wa kumtaka Davido kuuza hari lake.
Image: Instagram

Mchungaji mmoja nchini Nigeria amejitokeza akidai kwamba alikutana na Mungu kwenye ndoto na kumppa agizo la kumtaarifu msanii Davido kulipiga mnada gari lake jipya aina ya Maybach 2023, siku chache tu baada ya msanii huyo kulinunua gari hilo la kifahari.

Kwa mujibu wa video za nabii huyo ambazo zimekuwa zikienezwa mitandaoni, nabii huyo aliambiwa na Mungu kuwa hataki tena atumie Maybach yake mpya na kwamba anapaswa kuiuza.

Nabii alifichua haya kwenye video hapa chini kama ilivyoshirikiwa na Linda Ikeji blog kwenye Instagram.

"Mungu ainijia kwa ndoto kuhusu msanii mmoja mkubwa wa Nigeria, Davido. Aliniambia nimwambie asitumie gari ambalo amelinunua hivi majuzi na badala yake kuliuza. Usilitumie, liuze tu kwa sababu shetani ameamua kulitumia kukuangusha. Mungu amekubariki lakini shetani anataka kukuangusha," Alisema mchungaji huyo.

Davido hata hivyo bado hajajibu mafunuo ya mtu wa Mungu.

Mwezi mmoja uliopita, iliripotiwa kwamba msanii Davido alijinunulia gari la kifahari aina ya Maybach Virgil Abloh la 2023, moja ya magari 150 ya aina hiyo ambayo yalitolewa na kampuni hiyo kwa mwaka 2023.

Msanii huyo alitajwa kulinunua gari hilo kwa shilingi Zaidi ya milioni 110 za Kenya.

Msanii huyo amerejea kwa kishindo kikubwa kwenye muziki wiki chache zilizopita baada ya kuchukua kimya kirefu kufuatia kifo cha mwanawe Ifeanyi mwezi Novemba mwaka jana.

Mkuu wa DMW, ambaye amekuwa kwenye shamrashamra za ununuzi, alifichua kuwa alitumia kiasi cha dola milioni moja kwa siku moja tu.

Baadaye, inasemekana alitumia $400,000 zaidi kwenye saa ya Patek Philippe ili kukamilisha ununuzi wake wa hivi karibuni wa kifahari.