Ushauri wa Kamene Goro kwa warembo wanaotamani kutoka kimapenzi na Obinna

"Ukitaka Obinna akupende, usivute sheesha, bangi au sigara, usiombe pesa, penda watoto halafu pia kuwa mpenzi mzuri, na usikuje kwake kama una kucha mbovu," - Kamene alishauri.

Muhtasari

• Pia aliwashauri warembo kufahamu kuwa kama Obinna ameshakuamini, hufai kuanza kumwekea ulinzi na kumfuatafuata nyuma kama una wasiwasi naye.

Kamene Goro awashauri vidosho jinsi ya kumpata Obinna kimapenzi.
Kamene Goro awashauri vidosho jinsi ya kumpata Obinna kimapenzi.
Image: Screengrab//YouTube

Kamene Goro ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa mchekeshaji Oga Obinna amewashauri vidosho wanaolilia ngoa penzi la Obinna jinsi ya kulipata penzi hilo na kubwa Zaidi jinsi ya kuhakikisha kwamba penzi na Obinna linadumu.

Kwa mujibu wa Kamene, Obinna ni mtu mmoja ambaye huwahukumu warembo na kuwasoma tabia zao kutokana na maongezi yao.

Kamene alisema kuwa katika kipindi ambacho wamekuwa marafiki na Obinna, anafahamu fika kwamba mchekeshaji huyo ana pesa lakini hapendi warembo ambao ni wa kuongea kila mara, huku pia akiwashauri kutoweka ombi la pesa kutoka kwa Obinna iwapo wanataka wachumbiane naye, kwani atawapa tu mwenyewe bila kuombwa.

“Kitu kimoja ambacho mnafaa kujua, Obinna ni mtu ambaye atakuhukumu kutokana na maongezi yako. Kama wewe ni dem wa kuzungumzia vitu kama sheesha, unaanza kumuomba pesa… nisikilize, Obinna ana pesa, atakupa pesa lakini usimuombe. Si eti uanze kujifanya, beb hiyo uber utanilipia. Acha kabisa,” Kamene alishauri.

Pia aliwashauri warembo kufahamu kuwa kama Obinna ameshakuamini, hufai kuanza kumwekea ulinzi na kumfuatafuata nyuma kama una wasiwasi naye.

“Obinna anapenda mwanamke mwenye kichwa na fikira kama zake, kwa hiyo jifunze jinsi na kuwa na mzungumzo, jua nini kinaendelea duniani, sio kila kitu kitakuwa kuhusu vilabu na usikunywe pombe ukajisahau, usivute sheesha, bangi au sigara, usiombe pesa, penda watoto halafu pia kuwa mpenzi mzuri, na usikuje kwake kama una kucha mbovu,” Kamene alitaja baadhi ya vitu ambavyo warembo wanaootamani kutoka kimapenzi na rafiki yake Obinna wanafaa kuzingatia.