Crazy Kennar atangaza operesheni ya kutafuta mtu anayemfanana

Nchini Kenya, si jambo geni kwa mtu kujitokeza akimtafuta pacha wake, mwaka jana jamaa alijitokeza akilia vikali kuwa ni mtoto wa hayati Mwai Kibaki.

Muhtasari

• “Natafuta mtu ambaye anafanana kabisa na mimi. Tuma picha kwenye DM,” Kennar aliandika.

Crazy Kennar atangaza kumtafuta mtu anayemfanana.
Crazy Kennar atangaza kumtafuta mtu anayemfanana.
Image: Instagram

Mchekeshaji Crazy Kennnar amewashangaza wengi baada ya kutangaza operesheni ya kumtafuta mtu yeyote ambaye ana uhakika kwamba anafanana naye kumtafuta kwa kumtumia picha zake kwenye faragha zake mitandaoni.

Kennar aliandika haya kupitia instastory yake akisema kuwa anamtafuta mtu yeyote au mwanamke au mwanamume ambaye wanafanana naye kabisa, na kusema kuwa ikiwa kunaye mtu kama huyo, basi atume picha kwenye DM yake ili akague mwenyewe.

“Natafuta mtu ambaye anafanana kabisa na mimi. Tuma picha kwenye DM,” Kennar aliandika.

Hata hivyo, mchekeshaji huyo hakubainisha ikiwa tangazo hilo pia ni la watu wa ukoo wake ambao huenda wanalandana naye kwa njia moja au nyingine, au ni mtu ambaye anamfanana bila ya kuwa na uhusiano wowote wa damu au kiukoo.

Baadhi walihisi mcheshi huyo anatafuta mtu ambaye anamfanana ili kumjumuisha kwenye uigizaji wa video zake fupi za kuchekesha, lakini pia kuna baadhi waliohisi ni mzaha tu alikuwa anafanya.

Suala la watu kuwatafuta wale ambao wanahisi kufanana nao si geni humu nchini kwani miaka mitatu iliyopita kuna jamaa aliyejitokeza akisema anamtafuta Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kudai kuwa watu walikuwa wakimwambia anamfanana.

Mwaka jana pia alitokea mwanamume kutoka Bungoma ambaye alikuwa analazimisha kukutana na familia ya rais wa tatu Hayati Mwai Kibaki baada ya kifo chake.

Mwanamume huyo alizua tafrani katika majengo ya bunge akiomboleza vikali na kutaka kutambuliwa kama mmoja wa watoto wa KIbaki lakini alizuiliwa na vyombo vya usalala, katika shughuli ya kutizama maiti ya kiongozi huyo.

Lakini pia mwaka huo huo aliyekuwa mgombea urais George Wajackoyah alikutana na mwanamume mmoja kutoka mtaa wa Kibera ambaye alikuwa na mfanano sawia na wake na hata kumpa zawadi ya saa yake ghali.

Mwaka huu pia mwanamume mmoja amejitokeza miezi michache iliyopita akidai kufanana na mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na kutaka kupatana naye.