Mulamwah: Kwa sasa siko tayari kuwa na mwanamke juu niliachwa bila pesa

“Kwa Ruth K, Yeye ni bestee kwa sasa, kwa hiyo kama vitu vingine vitakuwa pengine huko mbele mbele, huwezi jua,” alisema.

Muhtasari

• Mulamwah hata hivyo hakuweza kufutilia mbali kabisa uwezekano wa kuchumbiana na mrembo Ruth K akisema;

• “Yeye ni bestee kwa sasa, kwa hiyo kama vitu vingine vitakuwa pengine huko mbele mbele, huwezi jua,” alisema.

Mulamwah asema hataki wanawake sasa hivi.
Mulamwah asema hataki wanawake sasa hivi.
Image: Facebook

Kwa mara nyingine tena, mchekeshaji wa mitandaoni Kendrick Mulamwah amenyoosha maelezo kuhusu rafiki yake wa Karibu Ruth K ambaye wanapenda kutaniana kwa msimbo ‘bestee bestee’ licha ya wengi kuhisi kuna kitu Zaidi ya urafiki wa kawaida.

Mulamwah ameweka wazi kwamba Ruth K atasalia kuwa rafiki yake wala hakuna kitu kinachondelea baina yao Zaidi ya urafiki tu, huku pia akimshukuru kwa kusimama upande wa faraja yake kila muda anapohitaji mtu wa kuzungumza na yeye.

Mchekeshaji huyo alisema kwamba kwa sasa hajui ni nini kitatoea huko mbeleni alipoulizwa iwapo anafaa kumpandisha hadhi Ruth K kutoka kuwa rafiki hadi kuwa mchumba, huku akisema kuwa hayuko tayari kabisa kuwa na mwanamke yeyote.

“Hakuna kitu poa kama kuwa na rafiki yaani bestee ni fiti kushinda kitu kingine chochote, ako kwangu kila muda kila siku. Lakini huwezi jua ya Mungu yamepangwa aje lakini kwa sasa mimi siko tayari kwa wanawake aina yoyote, sidai. Sasa hivi wacha float ipande,” Mulamwah alisema.

Akirejelea uhusiano wake na mama mtoto wake, Carrol Sonie ambao ulisambaratika miaka miwili iliyopita, Mulamwah alisema kuwa aliachwa bila kitu chochote kwa hiyo anahitaji muda Zaidi kujipanga kabla ya kujaribu kurejelea tena kwenye mduara wa mapenzi.

“Tuliachwa hatuna pesa wacha tufanye marekebisho kabla ya kurudi kwa huo uwanja. Bestee atulie afanye kazi, yeye amesainiwa chini ya Mulamwah Entertainment, naona anapiga kazi poa ako na endorsements, tunaendelea vizuri,” Mulamwah aliongeza.

Mulamwah hata hivyo hakuweza kufutilia mbali kabisa uwezekano wa kuchumbiana na mrembo Ruth K akisema;

“Yeye ni bestee kwa sasa, kwa hiyo kama vitu vingine vitakuwa pengine huko mbele mbele, huwezi jua,” alisema.