Jaymo Ule Msee ataka serikali kuweka ushuru kwa wachuuzi wa ngono

“Hiyo street mahali unauziwa, hizo taa nani ameweka? Lami nani ameweka? Mahali unauziwa hujanyonywa, nani anakupa usalama? Serikali inapoteza biloni 5 za ushuru kila siku," - Jaymo.

Muhtasari

• "Umeenda umesikilizana na mtu ni ngapi ndio nipige, ni elfu 5 sawa, unaweka kwa portal anareceive anawithdraw hapo ikiwa imekatwa ushuru" - Jaymo.

Jaymo Ule Msee ataka wachuuzi wa ngono kutozwa ushuru.
Jaymo Ule Msee ataka wachuuzi wa ngono kutozwa ushuru.
Image: Instagram

Mchekeshaji Jaymo Ule Msee ametoa pendekezo kwa serikali ya Kenya kuanzisha mchkato wa kuimarisha njia za kutoza ushuru biashara mbali mbali ambazo kama ilivyo sasa hazitozwi ushuru.

Katika mahojiano na SPM, Buzz, Jaymo alisema kuwa pesa ambazo kina dada wanatumiwa kununua bidhaa za urembo, nauli ya kuwatembelea wanaume wao ni baadhi ya pesa ambazo zinafaa kutozwa ushuru.

Alisema kuwa serikali kwa kila siku inapoteza angalau shilingi bilioni 5 kwa ushuru kutokana na miamala ambayo inafanywa kati ya wanaume kwenda kwa warembo wao pasi na kutozwa ushuru hela hizo.

Jaymo alipendekeza kwamba serikali inafaa ianzishe kitu kama portal ambapo mrembo akihitaji pesa jamaa anamuwekea pale na kabla mrembo hajazitoa, zinakuwa zimekatwa ushuru kwa asilimia Fulani.

Katika kile alisema kuwa kila mtu analipa ushuru kwa kutumia talanta yake, Jaymo alipendekeza kuwa hata wachuuzi wa ngono mitaani wanafaa kutozwa ushuru ili serikali ipate kutambua biashara yao na kuwalinda.

“Unajua kila mtu anatumia kipawa chake. Nyinyi mnalipa ushuru kwa sababu mnatumia akili, mtu kama Kipchoge analipa ushuru kwa sababu ya kutumia miguu yake… kila mtu anatumia sehemu Fulani ya mwili wake kufanya bishara. Kwa hiyo mbona wasilipe ushuru?” aliuliza.

“Hata hao wa mtaani wanafaa kulipa ushuru. Umeenda umesikilizana na mtu ni ngapi ndio nipige, ni elfu 5 sawa, unaweka kwa portal anareceive anawithdraw hapo ikiwa imekatwa ushuru ndio biashara yake pia ikuwe supported na serikali iweze kulinda hiyo biashara yake.”

“Hiyo street mahali unauziwa, hizo taa nani ameweka? Lami nani ameweka? Mahali unauziwa hujanyonywa, nani anakupa usalama? Ni hivyo, lazima tukuwe wajanja ili tupate ushuru. Tumefanya makadirio juzi na watu wa fedha pale tulipata kwa siku wanapoteza shilingi bilioni 5 za ushuru,” Jaymo alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa ni wakati sasa serikali ikuwe na ujanja Zaidi ijue kwamba kuna mianya mingi ambayo pesa zinapita bila kutozwa ushuru.