Brian Chira: Watu huniambia niko 'fluent' kwa Kiingereza, ndoto yangu ni kuwa mwanasosholaiti

"Awali nilikuwa nafanya uchekeshaji wa Kikuyu lakini haukuwa na mapokezi makubwa. " - Chira.

Muhtasari

• Licha ya wengi kusema kwamba nyingi ya video ambazo anazifanya kwenye TikTok mara nyingi huonekana mlevi, Chira alikanusha vikali dhana hiyo

Brian Chira
Brian Chira
Image: Screengrab

TikToker maarufu nchini Kenya Brian Chira ametaja sababu kwa nini mara nyingi hufanya skits zake za TikTok kwa lugha ya Kiingereza.

Katika mazungumzo na Oga Obinna, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika chuo cha Kabarak mjini Nakuru alisema kuwa kitambo alianza kwa kufanya video hizo kwa lugha ya Kikuyu lakini hazikuwahi kupata mapokezi mazuri.

Lakini pindi alipojaribu kuigiza kwa lugha ya Kimombo, mapokezi yalikuwa makubwa hadi baadhi ya mashabiki wake kuanza kumhimizia kuendelea kufanya skit hizo kwa Kiingereza katika kile walimshauri kwamba ana ufasaha mkubwa katika lugha hiyo.

“Nilipata umaarufu baada ya kutokea kwenye runinga kama shahidi mlevi wa ajali na baadae nilipotrend nilianza kufanya hivo kuwaonesha kwamba huyu ni yule kijana mliona kwa TV. Kutoka hapo nimekuwa nikifanya video kadhaa, kwa lugha ya Kimombo kwa sababu watu huniambia niko na ufasaha kwa Kiingereza. Awali nilikuwa nafanya uchekeshaji wa Kikuyu lakini haukuwa na mapokezi makubwa. Lakini sasa nilipokuja kupata nafasi ya kufanya kwa kimombo na watu wakakubali, nateleza nayo,” Chira alisema.

Licha ya wengi kusema kwamba nyingi ya video ambazo anazifanya kwenye TikTok mara nyingi huonekana mlevi, Chira alikanusha vikali dhana hiyo akisema kuwa yeye huwa hivyo na wengi wanamchukulia kama mlevi kumbe ndio hali yake tu.

Hata hivyo, Chira alisema kuwa ni kweli huwa anakunywa pombe lakini akasema si kila wakati kama ambavyo wengi wamejenga taswira kwenye vichwa vyao pindi tu wanapolisikia jina lake likitajwa.

Chira alisema kuwa ndoto yake ni kuwa mwanasosholaiti mkubwa nchini na ndio maana anaigiza katika video za ucheshi TikTok.