logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diana Marua asherehekea hatua mpya baada ya kupata wafuasi zaidi ya 900K kwenye Youtube

Mara ambazo video katika hiyo chaneli ilitazamwa huonyesha umaarufu wa chaneli.

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 July 2023 - 13:10

Muhtasari


  • • Mke huyo wa mwimbaji Bahati kwa sasa yuko katika furaha kupita wafuasi 900K kwenye YouTube, tangu ajiunge na jukwaa kubwa zaidi la kupakia video mnamo Agosti 19, 2019.
  • • Diana Marua ni miongoni mwa WanaYouTube wenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Kenya, kwani huwa anajikusanyia watazamaji kila anapopakia kitu kwenye Chaneli yake.
  • • Ingawa wafuasi wengi zaidi haimaanishi pesa zaidi kila wakati, hiyo ni ishara ya mamlaka ya chaneli.
Diana asherehekea hatua mpya baada ya kupata wafuasi zaidi ya 900K kwenye Youtube

Mwanablogu Diana Marua ni miongoni mwa WanaYouTube mashuhuri zaidi nchini Kenya, kwani amepiga hatua mpya  kwa kupata wafuasi 900K kwenye chaneli yake ya Youtube.

Mke huyo wa mwanamuziki Bahati kwa sasa yuko katika furaha kupita wafuasi 900K kwenye YouTube, tangu ajiunge na jukwaa kubwa zaidi la kupakia video mnamo Agosti 19, 2019.

Mama huyo wa watoto watatu, alienda kwenye mitandao ya kijamii kushukuru kwa mashabiki wake wote kwa kuunga mkono kazi yake kila mara na kuwa wafuasi waaminifu ambao wamesafiri naye kwa miaka mingi.

"Wapenzi wa Team Diana, Tazama jinsi tumetoka mbali. Msichana rahisi tu nina Mungu mkubwa na Timu inayoniunga mkono nyuma yangu.

Tuna wafuasi zaidi ya 900k na tuko rasmi kwenye #Barabarayawafuasimilioni 🥳. Kwa kila mtu ambaye anaunga mkono maudhui yangu na hata kwa wakosoaji wangu wote, tusingekuwa hapa bila nyinyi, ASANTENI!,” Diana aliandika.

Aliendelea kujigamba kwamba anailenga nafasi ya kwanza kama mtayarishaji wa maudhui aliye na wafuasi zaidi barani Afrika.

“Nambari 6 ya wabuni maudhui wa wanawake wanaofuatwa zaidi barani Afrika…. NAMBA 1, TUNAKUKUJIA 😎,” Marua aliongeza.

Diana Marua ni miongoni mwa WanaYouTube wenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Kenya, kwani huwa anajikusanyia watazamaji kila anapopakia kitu kwenye Chaneli yake.

Ingawa wafuasi wengi zaidi haimaanishi pesa zaidi kila wakati, hiyo ni ishara ya mamlaka ya chaneli.

Mara ambazo video katika hiyo chaneli ilitazamwa huonyesha umaarufu wa chaneli.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved