Eric Omondi amlilia Profesa Wangari Mathai kufufuka ili kuokoa miti

“Leo ni siku ya kuhuzunisha sana nchini, tunamkumbuka binti wa taifa leta Wangari Mathai. Mama amka mama.” Eric Omondi alikariri kwa huzini.

Muhtasari

• Eric alionekana kukariri shairi akihuzunika na kulia kwa kile kilichoenekana kuwa kuzungumza na nafsi ya marehemu Profesa Mathai kuwa kutokuwepo kwake ndio sababu ya miti nchini kuhukumiwa kifo.

Mchekeshaji Eric Omondi akimlilia Profesa Wangari Mathai.
Mchekeshaji Eric Omondi akimlilia Profesa Wangari Mathai.
Image: INSTAGRAM/ ERIC OMONDI

Mchekeshaji Eric Omondi amemlilia aliyekuwa mwanaharakati wa mazingira marehemu Profesa Wangari Mathai kufufuka ili kumshawishi Rais Ruto kufutilia mbali amri yake ya kuhalalalisha ukataji wa miti nchini.

Katika video aliyochapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, Eric alionekana kukariri shairi akihuzunika na kulia kwa kile kilichoenekana kuwa kuzungumza na nafsi ya marehemu Profesa Mathai kuwa kutokuwepo kwake ndio sababu ya miti nchini kuhukumiwa kifo.

“Leo ni siku ya kuhuzunisha sana nchini, tunamkumbuka binti wa taifa leta Wangari Mathai. Kutokuwepo kwake watato wake Miungu ya mvua wamehukumiwa kifo mbele ya umma. Mama amka mama.” Eric Omondi alikariri kwa huzini.

Jumapili, Ruto aliondoa marufuku ya takriban miaka sita ya kukata miti licha ya wasiwasi ulioibuliwa na wanaharakati wa mazingira. Ruto alisema hatua hiyo "ilicheleweshwa kwa muda mrefu" na inalenga kubuni nafasi za kazi na kufungua sekta za uchumi zinazotegemea mazao ya misitu.

“Hatuwezi kuwa na miti iliyokomaa inayooza kwenye misitu huku wenyeji wakiteseka kutokana na ukosefu wa mbao. Huo ni upumbavu,” alisema katika ibada ya kanisa huko Molo, mji ulio umbali wa kilomita 200 (maili 120) kaskazini magharibi mwa mji mkuu Nairobi.

"Ndio maana tumeamua kufungua msitu na kuvuna mbao ili tuweze kutengeneza ajira kwa vijana wetu na kufungua biashara."

Eric ameendeleza malalamishi yake kwa serikali ya Kenya kwanza kwa kile alihisi kuwa serikali hii ilikuwa inawafeli Wakenya baada ya Wabunge kupitisha na ata Rais Willima Ruto kutia sahihi mswada huo kuwa sheria.

Katika mahojiano na runinga ya KTN, Eric Omondi alisema kuwa serikali tawala ilisema kuwa itawakilisha watu maskini iliyowarejelea kuwa mama mboga na mtu wa bodaboda, ila, na kufikia zaidi ya miezi kumi sasa hakuna hata moja kati ya ahadi zake imetekeleza, kinachokusudiwa, ni gharama ya juu ya maisha inayochangiwa na kupanda kwa bei ya bidhaa.

Binafsi huu ndio mpango wangu kama Eric Omondi, unajua, petroli ikipanda kila kitu kitapanda bila shaka, wabunge pia wamewataliki Wakenya waliowachagua, wanaitumikia serikali, serikali yenyewe imekiri kuwa itawahudumia waliopigia kura mswada wa fedha 2023 wakikubaliana na mswada huo,” alieleza KTN.