logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ronaldo ashindwa kujizuia kunengua mauno kwenye gym akicheza wimbo wa Costa Titch

Ronaldo alionyesha vibe yake kwa wimbo wa Costa Titch - Ma Gang.

image
na Radio Jambo

Habari05 July 2023 - 11:45

Muhtasari


โ€ข Kwenye video hiyo, Ronaldo alikuwa anasikiliza wimbo wa msanii maarufu ambaye anatajwa kuwa mfalme wa Amapiano, marehemu Costa Titch, kwa jina Ma Gang.

 

Staa huyo alicheza densi ya Amapiano.

Staa namba moja wa soka ulimwenguni kutokea Ureno, Christiano Ronaldo amewakosha mashabiki wa muziki wa Amapiano wenye asili ya Afrika Kusini alipopakia video akichezo wimbo mmoja kwenye gym.

Ronaldo ambaye kwa sasa anakipiga zake Saudi Arabia kwa klabu ya Al Nassr aliapikia video akiwa kwenye gym kufanya mazoezi huku akiwa amevalia kaptura fupi na kifua wazi, ambapo alikuwa ananyanyua vyuma.

Kwenye video hiyo, Ronaldo alikuwa anasikiliza wimbo wa msanii maarufu ambaye anatajwa kuwa mfalme wa Amapiano, marehemu Costa Titch, kwa jina Ma Gang.

“Najisikia vizuri,” Ronaldo aliandika kwenye video hiyo.

Kwenda mwisho wa video hiyo baada ya kuhitimisha mazoezi yake ya kujenga misuli kwa siku, Ronaldo alionekana akijaribu kusakata densi kwa wimbo huo, huku akifanya kama anaiga jinsi msanii huyo aliyepanguka jukwaani na kufariki, alivyokuwa akinengua enzi za uhai wake.

Mashabiki wengi haswa wale wanaofagilia kazi za Costa Titch hawakuweza kudhibiti furaha yao na kumpa maua yake Ronaldo kwa kutambua kilicho bora.

“Ndugu zangu wa Afrika Kusini ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ kusanyika hapa ๐ŸŽถ๐ŸŽต” Pavel Vieira aliandika.

“Hii inanifanya nijivunie kuwa Mwafrika Kusini, natamani angeishi kuona hii ♥๏ธ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ"” Refeeq Domingo aliandika akionekana kurejelea marehemu Costa Titch.

“Hii inanifanya nijivunie kuwa Mwafrika Kusini, natamani angeishi kuona hii ♥๏ธ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ"”mwingine aliandika.

Ronaldo ndiye binadamu wa kwanza kabisa kuwahi kutokea tangu mtandao wa Instagram kuzinduliwa, ambaye ana ufuasi mkubwa Zaidi, hadi sasa akiwa na halaiki ya watu milioni Zaidi ya 590 ambao wanamfuata.

Kwa tathmini ya haraka tu, Ronaldo kuonesha video yake akisikiliza wimbo huo ni promotion kubwa tena ya bure ambayo aliupa wimbo huo kwa kionjo ambapo utawafanya wengi wa wafuasi wake kutaka kuufuatilia wimbo wenyewe kwenye majukwaa ya kidijitali na kuusikiliza wenyewe na hata kujaribu kutazama video kuona kama kweli Ronaldo aligonga ndipo katika kusakata densi au la.

Bilas haka, hii ni hatua kubwa kwa msanii huyo ambaye kwa bahati mbaya aliaga miezi michache iliyopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved