logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njugush ampiga JuaCali na kifaa kizito kichwani kwa kukejeli ucheshi wake

Njugush hatimaye amevunja kimvya chake na kuzungumzia kejeli za mwanamuziki Jua Cali.

image
na

Habari11 July 2023 - 08:17

Muhtasari


• Njugush alieleza kuwa sanaa inawafikia na kuwafurahisha watu tofauti tofauti  na haikuwa jukumu la kila mtu kufurahia kazi yake.

• Njugush alisema kuwa hawezi acha kufanya ucheshi na ata akafichua kwa wafuasi wake mpango wa kufanya kipindi cha 5 chaa TTNT.

Mwanamuziki Jua Cali na mchekeshaji Njugush.

Mchekeshaji maarufu Njugush hatimaye amevunja kimya chake na kuzungumzia kejeli za mwanamuziki Jua Cali.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini kutoka kwa ziara yake ya Austaralia,Njugush alisema kejeli za Jua Cali hazikumshtua kwani tayari alikuwa amepokea shutuma kutoka wa familia yake.

"Mimi nimeambiwa hivyo mpaka na familia, sasa watu sijui surely. Unajua alisema ni boy wangu, Jua Cali ata tumepatana na yeye mara moja pekee. Lakini hio ni maoni yake na inakubalika kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kuzungumza."

Njugush alieleza kuwa sanaa inawafikia na kuwafurahisha watu tofauti tofauti  na haikuwa lazia kwa kila mtu kufurahia kazi yake.

"Art is very subjective, wimbo unafurahishwa nayo mimi haitanifurahisha na hio haimanishi wimbo huo si mzuri. Ukweli kwamba wimbo unaoupenda hainifurahishi haimanishi si kazi nzuri."

Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alieleza juhudi alizoweka na vile ilikuwa ngumu kwake kufanikisha TTNT kuanzia kipindi cha kwanza adi sasa ambapo amefikisha kipindi cha nne. Kulingana naye kazi yake haiwezi anza kuwa mbaya wakati huu na alipokuwa akianza alikuwa sawa.

"TTNT 1, TTNT 2, TTNT 3, TTNT4 zote zilikuwa zimeuzwa tiketi zote, unafahamu vile ni ngumu kujaza ukumbi." Njugush alijivunia.

Baba huyo wa watoto wawili aliongeza kuwa alitambua mkono wa Mungu wake katika safari mzima ya kufanikisha kazi yake na pahali imefika kwake kuu ni kumshukuru na watu anaofanya kazi nao.

"Nafikiri ni Mungu tu, nimejaribu kufikiria ama kusema kuwa ni bidii yetu lakini kusema ukweli tu haya yote ni Mungu kwa hakika. Kisha baada ya Mungu ni kundi linalonishikilia mkono kina Butia, Abel Mutua na mke wangu mpendwa."

NJugush alisema kuwa hawezi acha kufanya ucheshi na ata akafichua kwa wafuasi wake mpango wa kufanya kipindi cha 5 chaa TTNT.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved