Hamisa Mobetto awapiga kiboko wanaosema soko ni chafu, amtambulisha mpenzi mpya!

"Zamani nilitaka watoto saba, lakini sasa hivi nataka watano. Tayari niko na watoto wawili, nimebakisha wengine watatu." - Hamisa Mobetto.

Muhtasari

• Hamisa Mobetto aliwafurahisha wafuasi wake kwa kushiriki video zilizoonyesha akiwa amemshika mkono mwanaume huyo ambaye bado hakuweza kubainika ni nani.

• Miezi kadhaa zilizopita kulikuwa na tetesi mitandaoni kuwa mpenzi huyo wa zamani wa Dianomd alikuwa kwenye mahusiano na rapa wa Marekani , Rick Ross.

Hamisa Mobetto na mpenzi wake mpya.
Hamisa Mobetto na mpenzi wake mpya.
Image: SNAPCHAT

Mwanasosholaiti maarufu nchini Tanzania, Hamisa Mobetto, amemuweka wazi mpenzi wake kwa umma baada ya kuweka uhusiano wao kuwa wa faragha kwa muda.

Katika sasisho la hivi majuzi kwenye akaunti yake ya Snapchat, Hamisa Mobetto aliwafurahisha wafuasi wake kwa kushiriki video zilizoonyesha akiwa amemshika mkono mwanaume huyo ambaye bado hatujaweza kubainisha ni nani.

"Kwa mwanaume huyu, nakupenda kushinda maneno yanavyoweza kueleza. Natumai kuwa utahisi upendo wangu ata kama sitakuwa karibu nawe kukuambia jinsi ninavyokupenda."

Baadaye Hamisa Mobetto alichapisha picha ya mwanaume huyo, akionyesha mwili wake wote. Ingawa alikuwa akitazama mbali na kamera.

Katika chapisho lingine, mama huyo mwenye watoto wawili wa baba tofauti alishiriki picha inayoonyesha jinsi mwanamume huyo alivyomzawadia shada la maua.

"Kwa mwanaume ambaye huwa ananiletea maua na vitu bora zaidi duniani . Bila shaka ninakupenda mpenzi. "

Mashabiki wamekuwa wakibashiri kwa hamu juu ya maisha yake ya mapenzi na kungoja kwa hamu kumwona mpenzi wake na sasa amewakatisha kiu.

Miezi kadhaa zilizopita kulikuwa na tetesi mitandaoni kuwa mpenzi huyo wa zamani wa Dianomd alikuwa kwenye mahusiano na rapa wa Marekani , Rick Ross.

Hamisa alijitokeza na kupinga kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi baina ya wawili hao akibainisha yao ilikuwa urafiki tu licha ya wafuasi wake kuhisi Rick Ross kudona.

Miezi miwili ilyopita katika mahojiano na PMTV, Mobetto aliweka wazi kwamba anatazamia kuolewa na kuongeza watoto.

Alisema anatazamia kuzaa watoto wengine watatu pindi baada ya kupata mwanaume wa kufunga ndoa naye. 

"Zamani nilitaka watoto saba, lakini sasa hivi nataka watano. Tayari niko na watoto wawili, nimebakisha wengine watatu. Wakati nikioelewa, mwaka wa kwanza napata mtoto mwingine," Mobetto alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa bongo Diamond Platnumz aliweka wazi kwamba hatapata mtoto mwingine kama bado hajajitosa kwenye ndoa.

"Sasa hivi sizai bila kuoelewa alisema," alisema.

Alisema ndoto yake ya kupata watoto wengi ilitokana na kuwa alizaliwa pekee yake katika familia yao.

"Mimi ni mtu ambaye anapenda watoto wengi. Nimezaliwa pekee yangu kwa hivyo mimi nataka niwe tofauti. Ningekuwa nimeolewa ningekuwa nimejaza nyumba," alisema.