logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Spice Diana ni mzuri wa kupata mtoto naye lakini sitamtafuna, ni ngoma tu - Diamond

Hata hivyo, Diamond alisisitiza kwamba hakuna uhusiano wa kimapenzi baina yao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 July 2023 - 12:29

Muhtasari


  • • Alifutilia mbali uwepo wa uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kusema kuwa muziki tu ambao wanafanya.
  • • “Kuhusiana na Diana tunaenda kufanya tu wimbo na sitamtafuna,” alisema.
Diamond amsifia Spice Diana

Diamond Platnumz yuko nchini Uganda ambapo anatarajiwa kutumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kololo usiku wa leo katika tamasha la vichekesho litakaloongozwa na mcheshi Alex Muhangi.

Msanii huyo alitua Uganda kwa kishindo akiwa na msanii mkongwe kutoka Kenya, Nameless na wengine wengi ambao watateka jukwaa la uchangishaji wa fedha kupitia tamasha la vichekesho.

Alhamisi alifanya mkutano na wanahabari katika hoteli moja alikotia nanga na aliweza kuwazungumzia wasanii mbali mbal iwa Uganda akiwemo Jose Chameleone na Spice Diana.

Diamond alisema kuwa anatamani sana kufanya kolabo na Chameleone lakini pia akafichua kwamba atatoa wimbo wake na Spice Diana kabla ya kurejea nchini Tanzania na hata ikiwezekana wafanye video na yeye kabla ya kuondoka.

Waandishi wa habari vile vile walimchokonoa kutaka kubaini ukaribu wa Spice Diana na lebo yake ya Wasafi ikizingatiwa kwamba amewahi fanya ngoma na Zuchu na pia Mbosso ambao wote ni wasanii walioko chini ya lebo ya WCB Wasafi.

Alifutilia mbali uwepo wa uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kusema kuwa muziki tu ambao wanafanya.

“Kuhusiana na Diana tunaenda kufanya tu wimbo na sitamtafuna,” alisema.

Diamond alichafua hali ya hewa kabisa na kusema kwamba ikiwa litatokea jambo kati yao basi hakuna atakayelaumiwa kwani wao ni watu wazima.

“Lakini ukweli ni kwamba Diana ni mrembo na ikitokea kitu kimetokea si makosa yangu wala si makosa yake kwa sababu sisi wote ni watu wazima. Ni msichana mrembo ambaye si vibaya kupata mtoto naye,” Diamond alisema.

Kali hiyo inakuja siku moja baada ya kuonekana na mrembo mwingine wakiwa wamebarizi kwenye kochi na wengi walisema anafanya makusudi kumuumiza Zuchu ambaye aliwahi kukiri kuwa ni mpenzi wake.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved