Hivi ni kweli 'ratecard' ya Khaligraph Jones haiwezi fikia ya Otile Brown? Coke Studio watajwa!

Otile alisema kuwa Coke Studio kwa muda mrefu wamejaribu kumfikia na kumpa nafasi ya kutumbuiza lakini wamekuwa wkaitofautiana katika pesa anazoziomba.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa Brown, Coke Studio hawakufikia kiasi cha hela ambazo alikuwa anataka ili kutumbuiza na ndio maana waliwachagua wasanii hao wengine wawili.

• “Hawaja wai fika bei , ever since … wachukue Hao wanaotaka kuenda,” Brown alijibu.

Image: Instagram

Msanii anayefanya vizuri Zaidi kutoka humu nchini katika miziki ya kizazi kipya, Otile Brown amerejea katika kazi ya muziki, ikiwa ni wiki moja tu baada ya kupata msiba wa kufiwa na mwanawe kichanga.

Brown aliachia kibao cha Confession akimshirikisha msanii kutoka Tanzania Atan na katika kukipiga promo kwenye Instagram yake, mashabiki walipata kukipa mapokezi mazuri na kumpa pongezi msanii huyo.

Lakini pia ikumbukwe Otile ambaye anafanya vizuri Zaidi ametoa wimbo huu kipindi ambapo kuna gumzo pevu haswa nchini kuhusu vigezo ambavyo Coke Studio walitumia kuteuwa wasanii wa kuwakilisha Kenya katika tamasha lao kuu lijalo.

Wiki jana, Coke Studio walitangaza kuwa Afrika Mashariki itawakilishwa na wasanii wawili tu, Khaligraph Jones na Nikita Kering’ – jambo ambalo lilivutia ukinzani mkali kutoka kwa wasanii walioachwa nje lakini pia mashabiki wa wasanii mbali mbali.

Msanii Willy Paul na Wakadinali waliteta vikali kuachwa nje licha ya kuwa ndio wasanii wanaotajwa kuwa vipenzi vya mashabiki humu nchini.

Lakini msanii mkongwe DNA aliwakosoa wasanii hao akisema kuwa Coke Studio ni chapa inayoangazia Zaidi masuala ya kifamilia na ndio maana waliwachagua wasanii wasiokuwa na kashfa hasi kwenye jamii.

Otile Brown naye amekuja na nadharia yake kuhusu mbona aliachwa nje na Coke Studio, ameyasema haya wakati alikuwa anamjibu shabiki mmoja Instagram aliyetaka Coke Studio kusasisha upya uteuzi wao.

Kwa mujibu wa Brown, Coke Studio hawakufikia kiasi cha hela ambazo alikuwa anataka ili kutumbuiza na ndio maana waliwachagua wasanii hao wengine wawili.

Hawaja wai fika bei , ever since … wachukue Hao wanaotaka kuenda,” Brown alijibu.

coke studio
coke studio

Wengi wanahisi Brown alifaa kuwa miongoni mwa chaguo za Coke Studio lakini kwa jibu la msanii huyo na iwapo ni kweli, basi kuna kidokezo kwamba huenda pengine walijaribu kumfikia ili kumpa nafasi hiyo lakini wakatofautiana katika kiasi cha pesa alizowatajia.