Mammito afuata mkondo wa Lupita, urembo bila nywele ndio mtindo!

Mammito alisema wanawake wenye vipara ndio hujua kupenda vyema.

Muhtasari

• Wiki tisa zilizopita, Lupita Nyong'o pia alitambulisha muoneako wake mpya, kichwa bila nywele.

Mammito afuata mtindo wa Lupita kunyoa upara.
VIPARA Mammito afuata mtindo wa Lupita kunyoa upara.
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji Mammito Eunice ametambulisha mtindo wake mpya wa bila nywele kwa mashabiki wake wa mitandaoni na kuwa mrembo wa hivi karibuni kuasi nywele na mitindo ya kusuka kwa kunyoa upara.

Kupitia Instagram yake, Mammito alipakia picha hizo akiwa amevalia nadhifu na kichwani upara ukiwa umeng’aa na kujishaua akisema kuwa mtindo bila nywele unamfaa na hana kesi ya kujibu kwa yeyote.

“Hakuna nywele hakuna DNA,” Mammito aliandika.

Mammito anatambulisha mtindo huo wiki chache tu baada ya muigizaji wa Kenya mwenye makao yake Mexico Lupita Nyong’o pia kutambulisha muonekano kama huo.

Lupita, ambaye ni mtoto wa gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o alipakia picha hiyo wiki tisa zilizopita na katika ujumbe ambao wote waliandika, walidokeza kwamba ni furaha tu kupunga upepo bila nywele.

Mammito alijisifia kwamba wanawake bila nywele ndio watu pekee hujua kupenda vizuri.

“Wanawake wenye vipara wanapenda Bora.”

Haya hapa ni maoni ya mashabiki wa Mammito baada ya kuwapa muonekano wake mpya;

“Ni Kutoa Mitindo ya Juu! Mrembo mpendwa ️” Polo Akinyi aliandika.

“New York! Paris! Huyu hapa Malkia anakuja kwenye Runway” Moyo Wangu alimtaka kujiunga katika siku ya fasheni kwenye majiji ya Ulaya.

“Ile kujiamini umejiamini mammito iko kwenye level nyingine😂” mwingine alimwambia.