Willis Raburu adokeza sababu ya kuondoka Citizen TV

“Unajua ukiwa pale ndani haikai ni kama unafanya kitu. Unajua uko peke yako, mpiga picha, timu, bosi wako... unazushiwa na unapongeza [ambayo ni mara chache sana]" - Raburu alidokeza.

Muhtasari

• Raburu aliondoka katika runinga ya Citizen wiki chache zilizopita na siku moja baadae akaachia kitabu chake lakini hakuweza kudokeza sababu ya kutoka katika runinga hiyo.

• Raburu alisema kuwa alianza kufikiria kujiuzulu kazi yake Citizen mwanzoni mwa mwezi Juni.

Raburu afichua kwa nini aliondoka Citizen TV
Raburu afichua kwa nini aliondoka Citizen TV
Image: FACEBOOK

Kwa mara ya kwanza, aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya Citizen Willis Raburu ametoa kidokezo ni kwa nini aliamua kuacha kazi hiyo yenye mshahara wa kutamanisha baada ya kufanya kwenye moja ya runginga kubwa Zaidi nchini kwa miaka 13.

Katika mahijiano na Director Phil kwenye YouTube, Raburu alisema kuwa japo hajajua kwa uhakika hatua yake ya baadae, lakini alitaka tu kujitengea muda wa kujitafakari mwenyewe – katika kile alisema kuwa kufanya kazi runingani kwa muda mrefu kwa kiasi Fulani kulimnyima uhuru Fulani ambao haupatikani ukiwa umeajiriwa.

Raburu alisema kuwa atatathmini kujiajiri mwenyewe katika mitandao ya kijamii ili kujifanyia kazi mwenyewe bila kuwekewa shinikizo kama lile ambalo alikuwa anapitia katika runinga ya Citizen.

“Unajua ukiwa pale ndani haikai ni kama unafanya kitu. Unajua uko peke yako, mpiga picha, timu, bosi wako... unazushiwa na unapongeza [ambayo ni mara chache sana] lakini hupati muda wako. Muda mwingi umejikita katika mambo ambayo yanaendelea, nani alikusalimia ofisini, bosi mwenye hakupendi, lakini hufikirii kuwa tunazungumza na watu milioni 3.5 kila Ijumaa usiku,” Raburu alisema.

Raburu aliondoka katika runinga ya Citizen wiki chache zilizopita na siku moja baadae akaachia kitabu chake lakini hakuweza kudokeza sababu ya kutoka katika runinga hiyo.

Raburu alisema kuwa alianza kufikiria kujiuzulu kazi yake Citizen mwanzoni mwa mwezi Juni.