Dadake Zari afichua maneno ya mwisho ya kuhuzunisha kwa mama yao kabla ya kufariki

Mamake Zari alifariki mwaka wa 2017 baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

Muhtasari

•Dadake alieleza kwa huzuni kile kilochotokea nyakati zake za mwisho akiwa na marehemu mama yao Halima Hassan.

• Zahara alidai katika kwamba mwezi wa Julai umekuwa mwezi mgumu zaidi tangu kifo cha mama yao.

Zari akiwa na mamake.
Zari akiwa na mamake.
Image: INSTAGRAM

Zahara Mohez, dadake Zari Hassan, amekumbuka nyakati zake za mwisho akiwa na marehemu mama yao Halima Hassan.

Julai 20, 2017, Halima alifariki dunia kutokana na saratani katika Hospitali ya Nakasero jijini Kampala, Uganda.

Dada yake Zari alielezea matukio yao ya mwisho wakiwa pamoja.

"Nilikuambia mama nipige kofi kama unasikia lakini majibu pekee niliyoyapata kutoka kwako yalikuwa machozi. Niliweka mkono wako juu ya shavu langu lakini ulikuwa umechoka na unaumwa sana.

Kitu kimoja nashukuru hata dakika zako za mwisho ulisimama na watoto wako na ukasema 'abana bang mwekume' siku zote tuwe pamoja na tusimame kwa kila mmoja na mama tunafanya hvyo haijalishi ni changamoto gani tunapitia tunashikamana daima. miss u so much."

Alidai katika chapisho lingine kwamba mwezi wa Julai umekuwa mwezi mgumu zaidi tangu kifo cha mama yao.

"Mama kukupoteza sikutegemea kuwa ingeweza kuuma siku zote za maisha yangu, siku zote niliomba nife mbele yako , nitakabiliana vipi na maumivu lakini uko mahali pazuri zaidi na kwa Mungu."

Mamake alipoaga, Zari alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii. Mama huyo wa watoto watano alishiriki habari hizo za kuhuzunisha na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yake;

"Ni kwa masikitiko makubwa mimi na familia yangu tunatangaza kifo cha mama yetu kipenzi aliyefariki asubuhi ya leo. Roho yake ipumzike kwa amani, Mwenyezi Mungu akusamehe madhambi yako na akupe Jana.

Zari aliongeza: "Utapendwa milele, sisi kama watoto wako tulipewa mwanamke bora kutoka kwa Mungu kama mama yetu. Tunashukuru yote uliyotufanyia. Tutakuenzi milele Mama. "