logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Esther Musila amwita mchawi mtu aliyemdunisha Guardian Angel kama 'house boy' wake

Mama huyo mwenye umri wa miaka 52 alienda kwenye sehemu ya maoni kumjibu shabiki huyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 July 2023 - 05:51

Muhtasari


  • • Esther Musila ni mwanamke wa aina hii ambaye hatoacha nafasi hata kidogo kwa mtu yeyote anayejaribu kumdunisha mumewe Guardian Angel.
Esther Musila, Guardian Angel wabemendana kwa mahaba

Kila mwanamke ambaye anampenda mumewe kwa dhati, dhamira ya kwanza akilini mwake ni kumtetea na kuipigania ndoa yake dhidi ya dhoruba za maneno kutoka kwa walimwengu.

Esther Musila ni mwanamke wa aina hii ambaye hatoacha nafasi hata kidogo kwa mtu yeyote anayejaribu kumdunisha mumewe Guardian Angel.

Musila katika video ya hivi karibuni kwenye TikTok, alilazimika kuweka Amani kando na kuchagua vita na ugomvi dhidi ya mtumizi mmoja wa mtandao huo aliyemdunisha mumwe Guardian Angel kwa kumuita kuwa ni kijakazi wa nyumbani kwa mwanamke huyo mkwasi.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 52 alienda kwenye sehemu ya maoni kumjibu shabiki aliyemtaja kwa kejeli Guardian, ambaye ni mdogo kwa miaka 20, kama "houseboy."

Katika kile kilionekana kama kumcukiza na kumghasi Musila, mtumizi huyo wa TikTok alisema kwamba Guardian Angel ni kama kijakazi wa Musila na kuwa alikuwa amemaliza kazi za ndani.

“Kijakazi wa ndani sasa amemaliza kupika na anajitayarisha kuazna kufua,” mtu huyo aliandika.

Kwa sauti ya hasira, Musila alisema kuwa hiyo ni chuki ambayo itampeleka pabaya mtu huyo anayeshinda akikosoa penzi lake kwa mumwe.

“Watu wangu nimeshawaambia, chuki na wivu, next level ni wewe kuwa mchawi. Tafadhali punguza chuki, punguza wewe…” Musila alijibu.

Mashabiki wengi walimsifu Esther kwa kumtetea mumewe. Licha ya ukosoaji huo, mama huyo wa watoto watatu amebaki bila wasiwasi na hana msamaha, akionyesha kuwa haogopi kutetea mapenzi ya maisha na familia yake.

Hadithi ya mapenzi kati ya wanandoa imekuwa mada ya kuvutia umma, na pengo lao la umri mara kwa mara likivutia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved