Pengine ningembeba Flaqo miezi 9 angenisaidia - Shangazi wa Flaqo

"Flaqo ako na mama yake na anasaidia mama yake peke yake." Alieleza mwanamke huyo anayedai kuwa shangazi ya Flaqo.

Muhtasari

โ€ข Mwanamke anyedai kuwa shangazi wa mchekeshaji Erastus Ayieko almaarufu Flaqo Raz amedai kuwa hapokei msaada wowote kutoka kwa mcheshi huyo.

โ€ข Mwanamke huyo ambaye bado jina lake halijabainishwa, alielezea Wafuasi wake katika akaunti yake ya TikTok jinsi anavyohusiana na mcheshi huyo.

Mchekeshaji Flaqo Raz
Mchekeshaji Flaqo Raz
Image: Instagram

Mwanamke anyedai kuwa shangazi wa mchekeshaji Erastus Ayieko almaarufu Flaqo Raz amedai kuwa hapokei msaada wowote kutoka kwa mcheshi huyo.

Kulingana na mwanamke huyo, Flaqo humsaidia mama yake peke yake na hata kumfanyia maendeleo katika shamba la mama yake na kuacha boma lake ambalo linapakana na la mama yake.

"Flaqo ako na mama yake na anasaidia mama yake peke yake. Mimi ni mama yake mdogo tu na nikikuja kwenu kuomba msaada msiniambie mambo ya Flaqo. Huyu kijana amewekea mama yake stima na kwetu hakueka na tuko majrinani tu hapo. Yaani kwa mama yake kuna stima na kwa nyuma yangu hakuna stima."

Mwanamke huyo ambaye bado jina lake halijabainishwa, alielezea Wafuasi wake katika akaunti yake ya TikTok jinsi anavyohusiana na mcheshi huyo.

"Achani niwaambie tu ukweli yote, Flaqo ni mtoto wangu, Mamaa yangu alikuwa mke wa pili na mama ya Flaqo alikuwa mke wa kwanza. Otis hawezi nisaidia kwa sababu si mimi niliyemzaa. Lakini kila kitu Flaqo anafanya anatumia tu sauti yangu."

Mpenzi huyo wa Sosholaiti Keranta mwaka jana alikuwa akiugua ugonjwa wa msongo wa mawazo na ugonjwa huo ulimlazimu kuchukua muda bila kuunda maudhui.

Alisema kuwa alikuwa maarufu akitengeneza pesa lakini hakuwa na furaha sana, na hakuna kitu kilichokuwa kikimsisimua. Wakati mwingi kulingana na Flaqo alikuwa akijipata mpweke na kumwaga machozi.

"Nakumbuka nilimaliza shoot, nakuwa na hisia fulani,Bien anajua, nilimpigia Bien simu nikaanza kusema mambo hata hayana maana,alinipa namba ya simu ya mtaalamu, ilikuwa hisia fulani sijui niseme Bipolar au Depression, nimekuwa nikipigana na hayo kwa mwaka mmoja sasa," Alieleza Flaqo.