Msanii Bahati alijipata katika kipindi cha aibu mbele ya mkewe na watoto wake katika sebule yao baada ya bintiye kumgonga kimakosa katika sehemu zake za siri.
Wanafamilia hao walikuwa na kikao cha mchezo wa chemsha bongo na masharti ya mchezo huo yalikuwa kwamba wa kupoteza swali alikuwa anapakwa unga usoni kwa kuinamishwa kwenye sinia lililokuwa limejazwa unga mezani.
Bahati alimuuliza Diana kuhusu kijakazi anayependelewa Zaidi na mwanawe Majesty kati ya vijakazi wawili wa nyumbani kwao.
Diana alikosea jibu ambalo Majesty alikataa na kushirikiana na babake kumpaka kwa lazima uso mama yake.
Kitendo hicho japo kilifurahiwa na Majesty na babake, kwa upande wa pili binti Heaven hakukiridhia na alijaribu kuwazuia dhidi ya kumpaka mamake unga usoni.
Katika mchakato wa kuwazuia wasimpake unga mama yake, Bahati na Majesty hata hivyo walifaulu kumpaka Diana unga na Heaven akajipata amemgonga kofi Bahati kwenye ‘kabati’ lake.
Bahati aliruka juu kama punda aliyeumwa na nyuki huku kwa haraka mkono wake wa kushoto ukifika kwenye nyeti na kushika kwa kupapasa kama njia moja ya kupoza uchungu.
“Eeei eeei eei, unanipiga sehemu?” Bahati alimuuliza kwa mshangao wa kila mtu huku akionekana kuwa na hamaki usoni na kutaka kuinama akiwa amejishika ‘kabati’ lake.
Awali, Bahati alikuwa wa kwanza kupata adhabu hiyo ya kulambishwa unga usoni baada ya kufeli kujibu kuhusu jina la mwalimu wa darasa wa mwanao Majesty.
Wakati huo, binti yake Heaven alikuwa anashinikiza uso wa babake kutumbukizwa katika sinia la unga huku Majesty akionesha pingamizi kali.
Kwa uchanganuzi wa haraka wa familia hiyo kutokana na kilichoonekana kwenye video hiyo, Binti Heaven anampenda na kumjali pakubwa mamake huku mvulana Majesty akisimama upande wa babake na hata kumhurumia kwa kumpangusa unga usoni, na pia kujaribu kuzuia asipakwe unga.