logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diana ammwagia Bahati unga usoni kwa kukosa kujua mwalimu wa mwanawe Majesty

Wanafamilia hao walikuwa wanashiriki mchezo wa chemsha bongo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 July 2023 - 05:33

Muhtasari


  • • Sharti la mchezo huo wa chemsha bongo ni kwamba mtu aliyekosa kujibu kwa ufasaha alikuwa anapakwa unga usoni.
  • • Bahati na familia yake wana mazoea ya kushiriki mchezo wa chemsha bongo mara kwa mara.
Bahati amwagiwa unga usoni kwa kutojibu swali la Diana

Msanii Bahati amelazimika kukubali kudhalilika mbele ya mkewe na mwanawe Majesty baada ya kufeli kujibu swali kuhusu mwalimu wa darasa wa mwanawe huyo.

Wanafamilia hao walikuwa wanashiriki mchezo ambapo Diana alikuwa na kadi za maswali mkono ni huku kwa upande mwingine Bahati akiwa ameketi kwenye kiti moto cha kujibu maswali hayo.

Kando yao kulikuwa na mwanao Majesty na ndiye alikuwa anathibitisha majibu ya babake kama ni kweli ama amenoa.

Iwapo angeotea, Bahati angelazimika kulambisha uso unga kama adhabu ya kufeli  kujibu swali kwa ufasaha.

Diana alimuuliza Bahati kuhusu jina la mwalimu wa darasa wa Majesty na Bahati, kama tu baba wengi ambao jukumu lao huishia tu katika ulipaji karo na si kufuatilia kujua mwalimu anayemfunza mwanawe, alishindwa kujibu na mwanawe akamchekelea na kumpaka unga usoni.

“Nitajie jina la mwalimu wa darasa wa Mejesty?” Diana alimuuliza Bahati.

Bahati alishangaa swali hilo ambalo hakuwa analitarajia na kuishia kwa kutaja jina tofauti ambalo hata hivyo Majesty alikanusha vikali na kumchekea babake akimwambia mwalimu huyo aliyemtaja aliondoka katika shule yao muda mrefu umepita.

Majesty alizidi kudhalilisha babake kwa kumtajia jina la mwalimu wao wa darasa wa sasa, na kumlazimu kusalimu amri ya kupakwa unga usoni.

Majesty pindi baada ya kumpaka babake unga usoni, alijihisi vibaya na kujuta akitaka kumpangusa unga ule lakini Diana alimwambia kwamba hafai kumpangusa kwani ni adhabu ya kukosa kumjua mwalimu wake wa darasa.

Bahati na familia yake wana mazoea ya kushiriki mchezo wa chemsha bongo mara kwa mara na kuonesha jinsi kila mmoja anajua suala fulani kuhusu familia yao kutoka kwa mali wanayomiliki, maendeleo ya wanao kimasomo, taaluma zao na maisha kwa ujumla.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved