Baada ya mtangazaji Willis Raburu kutangaza kuondoka katika runinga ya Citizen baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka 13, Hatimaye, runinga hiyo imepata mtu atayeichukua nafasi yake, na mtu huyu si mwingina ila ni mchekeshaji, Oga Oninna.
Akitangaza kwa bashasha kuu kupitia akaunti yake ya Instagram, Obinna alibainisha hii ilikuwa ndoto yake kuu kuanzia alipokuwa mtoto mdogo kuwa mtangazaji katika runinga ya Citizen.
“Ni heshima kuu kuwatangazia. Nimeishi kutamani kufanya kazi katika runinga ya Citizen na hatimaye, ndoto yangu imeweza kutimia. Usiku wa Leo nitaweza kuwa mtangazaji wa shoo kubwa barani 10/10. Mama we made it!”
Muunda maudhui huyo alisema ataweza kutumia uzoefu wake wa utangazaji katika shoo mbalimbali nchini kutekeleza majukumu aliyopewa. Aliwahakikishia mashabiki wake kuwa ameafikia matarajio yao.
Mnamo tarehe 26 mwezi Juni Mtangazaji wa Citizen TV, Willis Raburu alitangaza kuondoka katika runinga hiyo baada ya kuhudumu kwa muda wa takriban miaka 13.
Katika video alizochapisha katika akaunti zake za mitandao ya kijamii, Willis alitangaza uamuzi wake kuondoka na kusema haikuwa rahisi kwake.
"Nimefanya uamuzi wa kuondoka Royal Media Services na imekuwa uamuzi mgumu sana kwangu."
Baba huyo wa watoto wawili alifichua kuwa aliweza kuwasilisha barua ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Juni na shirika hilo lilipokea habari hizo vyema na kuweza kumsaidia katika safari ya kuondoka.
"Tangu nilipowasilisha barua ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Juni mpaka sai wamekuwa watu wazuri kwangu katika mapito haya."