Ni furaha ya kila mama kumuona mwanawe akiwa anatabasamu; kila mama anataka kuona tabasamu katika uso wa binti yake haswa anapompata mpenzi.
Akothee ni mama wa aina hiyo ambaye hachoki kufurahia maisha ya mabinti zake wakubwa ambao sasa wana uhuru wa kutoka kimapenzi na wanaowapenda.
Msanii huyo alipakia klipu ya mchezo mmoja wa kuhatarisha ambao binti yake mdogo Fancy Makadia alikuwa anashiriki na mpenzi wake.
Makadia na mpenzi wake walionekana kuwa katika chombo kimoja cha kielektronini wakiwa wamelala juu ya chombo hicho kiocho kama jahazi huku kila mmoja ameshikilia kwa nguvu wakitelezeshwa katika kile kilionekana kama ni theluji kwa kasi ya ajabu.
Akothee aliwapa mashabiki wake kionjo cha mchezo huo na kufurahia jinsi binti yake alikuwa anapunja maisha na mpenzi wake, lakini pia akaonesha wasiwasi wake kama mama kuhusu mchezo huo ulionekana kuwa wa kuhatarisha maisha.
Mama huyo wa watoto watano alimuusia Makadia kuwa makini katika mchezo wake na mpenziwe, haswa baada ya klipu hiyo kumalizia ikimuonesha akianguka kutoka kwa chombo hicho na kugaragara kwa kasi kweney sakafu ya theluji.
“Kuzaa ni kama kuruhusu moyo wako kuondoka kwenye ubavu wako. Tazama huyu mkwe wangu amemchukua binti yangu pia. Oyaaa, tafadhali abeg, huyo ni mtoto wangu wa mwisho wa kuzaliwa wa Kiafrika nichungie tafadhali Mhandisi @fancy_makadia mchezo gani huu π€π€π€π€π€ Sasa ukivunjika shingo utasema nini? Ati mapenzi yana run dunia, Dunia gani?” Akothee alisema.
Mashabiki wa Akothee walioona mchezo huo hatari walitoa maoni tofauti, wengine wakisema kuwa angekuwa ni yeye na mumewe Omoshi wala asingejali kuhusu usalama wa shingo.
Wengine walisema kuwa wasiwasi ndio akili, wakisema kuwa hawawezi ruhusu wanao kushiriki katika michezo kama hiyo.
βMama ni Mama moyo wangu uliruka hii hapanaβ mama mmoja alisema.
βπππππInge kua ni ww na omoshi uwenzi sema mambo na shingoπππβ mwingine alimtania.
βππππ hii inatisha ingawa ππβ momo Nanjumba alisema.
Wewe ungeruhusu mwanao kushiriki katika mchezo kama huu?