logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Huwa simwambii Bobi cha kufanya; Ninamfuata tu kama shabiki - Barbie, mkewe Bobi Wine

Katika mkutan huo, Bobi alizungumzia kilichomsukuma kuingia kwenye siasa 2017.

image
na Davis Ojiambo

Burudani30 July 2023 - 05:32

Muhtasari


  • • Bobi Wine alisafiri hadi Marekani pamoja na mke wake na watoto kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo inayoorodhesha matukio ya hatari ya uchaguzi mkuu wa 2021 nchini Uganda.
Bobi Wine na mkewe Barbie Kyagulanyi

Barbie Kyagulanyi, mumewe mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda amefunguka kwamba hajawahi mfanyia maamuzi ya ni nini cha kufanya mumewe.

Alisema haya katika hafla ya kutazamwa kwa mara ya kwanza filamu moja nchini humo ambapo alisema kuwa hajawahi mchagulia Bobi Wine cha kufanya na hata wakati aliamua kuingia katika siasa, Barbie hakumpa ushauri wa kumkataza wala kumwambia aendelee.

Barbie alisema kwamba yeye kwa mumewe ni kama shabiki tu na siku zote humfuata nyuma kama ambavyo mtu yeyote anafanya.

Katika onyesho la filamu mpya ya hali halisi ya National Geographic kuhusu kiongozi wa NUP huko Los Angeles, Barbie aliulizwa kama alifikiria kumzuia kuhatarisha maisha yake katika kupigana na Serikali ya Uganda.

"Mimi ni shabiki wa Bobi Wine," alisema kwa hadhira iliyopakia. “... na sisi mashabiki wa Bobi Wine tunakwenda tu Bobi Wine anapokwenda."

Barbie alikwenda kuelezea mumewe kama mtu  "asiyetabirika sana."

“Huwezi kujua atakuwa wapi kesho; Kwa hivyo huwa sifikirii chochote anapoamua kukifanya. Hainihusu mimi, huwa inahusu watu na mimi ni miongoni mwa watu hao.”

Barbie alisema hata hivyo, kwamba hakushangaa kuona umati mkubwa wa watu ukimfuata mumewe “kwa sababu alikuwa mdogo na alizungumza lugha ya vijana.”

Kwa upande wake, Bobi Wine aliiambia hadhira kwamba alichukua uamuzi wa ghafla wa kuanza kuelekea siasa, baada ya kushambuliwa usiku mmoja kwenye baa.

Kiongozi huyo wa upinzani alisimulia mara nyingi jinsi alivyojiona kuwa hawezi kuguswa katika kilele cha kazi yake ya muziki, hadi alipovamiwa na kupigwa ngumi bila msaada na mtu aliyekuwa na silaha, aliyeunganishwa sana na viongozi wakuu serikalini.

Hilo anasema, ndilo lililomsukuma kuanza kuweka nje muziki wenye cheche za kisiasa, na hatimaye kumtia katika siasa mwaka wa 2017.

Bobi Wine alisafiri hadi Marekani pamoja na mke wake na watoto kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo inayoorodhesha matukio ya hatari ya uchaguzi mkuu wa 2021 nchini Uganda.

Inajumuisha zaidi ya saa 4000 za video mbichi ambazo zilinaswa wakati wa msimu wa uchaguzi na zimehaririwa na kubanwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved