Azziad: Mafanikio yangu yalikuja baada ya kazi ya miaka mingi, si kwa sababu ya video ya TikTok

“Nathani watu hawawezi kufahamu safari yangu kabla ya umaarufu, nilianza kazi yangu tangu nilipozaliwa," Azziad alisema.

Muhtasari

• Kulingana na Azziad, alianza kazi yake tangu alipokuwa mdogo na watu wanaomfahamu vyema wanajua umaarufu wake haukuwa mafanikio ya haraka bali ilikuwa kazi ya takriban miaka 14.

Azziad Nasenya
Image: Facebook

Mwanatiktok almaarufu Azziad Nasenya amefichua kuwa umaarufu wake haukutegemea video aliyofanya ya muziki wa Mejja ‘Utawezana’, bali ilikuwa bidii ya zaidi ya miaka 20.

Kulingana na Azziad, alianza kazi yake tangu alipokuwa mdogo na watu wanaomfahamu vyema wanajua umaarufu wake haukuwa mafanikio ya haraka bali ilikuwa kazi ya takriban miaka 14.

“Nathani watu hawawezi kufahamu safari yangu kabla ya umaarufu, nimeshuhudia watu wengi wakisema nilipata umaarfu wa haraka lakini kusema ukweli mimi naye nilianza kazi yangu tangu nilipozaliwa. Na nikiwa mdogo sikufahamu kuwa ningefika hapa, na nikitafakari naona enyewe ndio maana niko hapa.” Azziad alieleza wakati wa mahojiano na mtayarishaji wa filamu Phil Director.

Azziad alieleza kuwa amekuwa akiigiza kuanzia alipokuwa katika shule ya msingi na kuendeleza taaluma yake katika chuo kikuu ambapo aliweza kutuzwa kama muigizaji bora wa kike katika mwaka wake wa kwanza katika chuo kikuu.

“Nilikuwa nikiigiza nikiwa shule ya msingi na pia shule ya upili na nilikuwa form four peke yake alikubaliwa kuigiza wakati huo shuleni kwetu. Na ata nilipojiunga na chuo kikuu niliendelea kuigiza na nikaweza kupata tuzo za muigizaji bora nikiwa fresher bana.”

Azziad alipata umaarufu mkubwa mwaka wa 2020 akiwa na umri wa miaka 19 baada ya video yake akinengua mauno, kwa wimbo wa mejja akimshirikisha Femi One ‘Utawezana’, kuenea mitandaoni.

Umaarufu na kazi yake katika tasnia pana ya burudani iliweza kutambuliwa adi na waziri wa spoti, Ababu Namwamba. Waziri huyo alimteua Azziad pamoja na watumbuizaji wengine nchini ikiwa ni pamoja na Churchill.