Rotimi aburuzwa mitandaoni kwa kum'cheat Vanessa Mdee na mchekeshaji wa USA

Rotimi alikuwa kwenye jukwaa akitumbuiza na mrembo huyo akaibukia kutoka kwa umati na kuanza kukinogesha mbele ya Rotimi akichukua mkono wake na kushika paja la Rotimi akitaka kumvuta.

Muhtasari

• Lakini wanoko na wakuda mitandaoni kama kawaida walihisi msanii huyo hakufanya vizuri.

• Wengine walihisi ni sawa kwa kile kilichotokea, wakisema kwamba ni kazi ya Sanaa tu na wote ni watumbuizaji.

Vanessa Mdee na Rotimi kwa video
Vanessa Mdee na Rotimi kwa video
Image: Instagram

Msanii wa Marekani Rotimi ambaye ni shemeji wa Afrika Mashariki kuwa uhusiano wake na msanii Vanessa Mdee ametiwa kwenye kikaango mitandaoni baada ya video kuibuka mitandaoni akicheza kwa njia ya ukakasi na mchekeshaji wa Marekani B S     imone.

Video hiyo ambayo ilipakiwa na blogu za udaku maarufu nchini Marekani ikiwemo Hollywood Unlocked na The Showroom inamuonesha Rotimi akiwa kifua wazi huku mrembo huyo akicheza densi mbele yake kwa kumgusisha makalio.

Rotimi alikuwa kwenye jukwaa akitumbuiza ambapo alikwenda bila shati na mrembo huyo akaibukia kutoka kwa umati na kuanza kukinogesha mbele ya Rotimi na kwa wakati mmoja alionekana akichukua mkono wake na kushika paja la Rotimi akitaka kumvuta karibu naye Zaidi.

Hata hivyo, Rotimi, baba wa watoto wawili na Vanessa Mdee alikuwa makini kutotoa picha mbaya itakayomkera mkewe na mashemeji nyumbani kwani alionekana kabisa kulinda mstari wake asije akauvuka na kangaja huenda yakaja.

Lakini wanoko na wakuda mitandaoni kama kawaida walihisi msanii huyo hakufanya vizuri Zaidi kujizuia dhidi ya densi ya ukakasi ya mchekeshaji B Simone na walikuwa wepesi kumshtumu wakisema kuwa amemkosea mkewe kwa kukubali kuchezeshewa makalio na mwanamke mwingine jukwaani hali ya kuwa yeyey badi ni mume wa mtu.

Wengine walihisi ni sawa kwa kile kilichotokea, wakisema kwamba ni kazi ya Sanaa tu na wote ni watumbuizaji, wakiongeza kwamba hata hanaoana na Vanessa bali ni kwamba wana watoto pamoja.

Haya hapa ni baadhi ya watu kutoka kwa kurasa za blogu hizo Instagram;

“Aliifanya vizuri mrembo huyo, hata hawakutagusana,” Winnie winnjie alisema.

“Kwa hiyo ana ruhusa ya kucheza hivyo kwa mwanamume aliye oa?” glammed by Monasia

“Nadhani ameoa ama ana mchumba” Mz Truebeauty alishangaa.

“Hivyo ndivyo watu mnafaa kuchezeana densi wakati mnajua kila mmoja wenu ana mtu, naipenda hii yao,” Dr Tee boogie aliwapongeza.

“Huyo msichana anavuka sana, nadhani Rotimi ni mume wa mtu” mwingine aliguna.

“Mtu yeyote anayeona ubaya katika densi hii ya kawaida unafaa kufyata ulimi,” Real Modeltype alisema.

 

Hata hivyo, Rotimi na Vanessa wote walifika kwenye video hiyo iliyochapishwa na B Simone na kutoa maoni yao, Vanessa akionekana kutokuwa na shida na densi hiyo huku Rotimi akisema kwamba katika siku 30 zijazo ataachia ngoma mpya.

“Well Belize, tumeifanya hatimaye. Tumemaliza kufanya tamasha kwenye showroom. Taarifa za pembeni ni kwamba nina wimbo mpya unakuja ndani ya siku 30,” Rotimi aliandika.

Kwa upande wake, Vanessa alionekana kutokuwa na tatizo na video hiyo akisema kwamba tayari ameshamwambia Rotimi aipate kutoka kwa B Simone ili aipakie mwenyewe kwenye kurasa zake.

“Wakati huo huo mimi nishamwambia mpenzi wangu aipate video hii kutoka kwa B Simone ili niichapishe mwenyewe. Una vibe sana dada,” Vanessa aliandika akimpongeza B Simone.

Kwa upande wake pia, B Simone alisema kuwa hakuwa tayari kwa densi hiyo nak usema alivutwa jukwaani na Rotimi akimtaja kama kaka yake.

“Walinivuta jukwaani na kaka yangu Rotimi, nilikuwa na wasiwasi sana, nilijiambia ‘kuwa makini ili usianguke’” B Simone aliandika.

Hii hapa video hiyo;