Mr. Seed amshukuru mkewe kwa kumsadia baada ya kupata ajali mbaya

"Nakushukuru sana na pia asanti sana kwa kuwa upande wangu nikiwa mgonjwa. Na hata hio time nilikuwa na depression bana but hakuniacha." Mr Seed alitoa shukrani zake.

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo alibainisha kuwa mpenzi wake alikuwa nguzo muhimu katika safari yake ya kuuguza majeraha ya mwili pamoja na unyongovu kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya ajali.

• Mnamo April 29 mwaka huu, msanii huyo wa zamani wa EMB records aliponea kifo chupuchupu baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya Nairobi-Nanyuki.

Mwimbaji Mr Seed amshukuru mke wake kwa kusalia naye na kumsaidia katika safari yake ya matibabu baada ya ajali mbaya ya barabarani.
Mwimbaji Mr Seed amshukuru mke wake kwa kusalia naye na kumsaidia katika safari yake ya matibabu baada ya ajali mbaya ya barabarani.
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa nyimbo za Injii, Moses Tarus Omondi almaarufu Mr Seed amemshukuru mpenzi wake, Nimo Gachuiri kwa kusalia naye na kumsaidia kuweza kupona kutoka kwa majeraha mabaya aliyopata baada ya ajali mbaya ya barabarani.

Mwanamuziki huyo alibainisha kuwa mpenzi wake alikuwa nguzo muhimu katika safari yake ya kuuguza majeraha ya mwili pamoja na unyongovu kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya ajali.

"Nakushukuru sana na pia asanti sana kwa kuwa upande wangu nikiwa mgonjwa. Na ata hio time nilikuwa na depression bana but hakuniacha. Hio time nlikuwa nafeel sina maana yoyote kwa maisha yangu na kusema ukweli umekuwa nguzo muhimu sana kama haungekuwa wakati huo ata sijui ningefanya nini," Mr Seed alishuru mpenzi wake.

Mwimbaji huyo wa injili pia alimshukuru mtayarishaji wa muziki J Blessigs ambaye kulingana na Seed amekuwa kama mzazi kwake. 

Mnamo April 29 mwaka huu, msanii huyo wa zamani wa EMB records aliponea kifo  baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya Nairobi-Nanyuki.

Kwa bahati mbaya, ajali hiyo ilipokonya uhai wa moja wa rafiki yake na mwenzake kazini, mpiga video Ambrose Khan ambaye alizikwa mwezi Mei.

Marehemu Ambrose alikuwa kwenye gari moja na Mr Seed, DK Kwenye Beat, mpiga picha mwingine na mfanyabiashara wakati wa ajali.Yeye ndiye mtu pekee aliyekuwa kwa gari hilo ambaye alipoteza maisha huku wengine wawili waliokuwa kwa gari ambalo waligonga nalo wakifariki dunia pia.

Mr Seed na wenzake walionusurika walipata majeraha mwilini, ambayo mwimbaji huyo wa kibao 'Dawa ya Baridi' bado hajaweza kukabiliana nayo kikamilifu. Hata hivyo amepata maendeleo makubwa kiafya tangu ajali hiyo kutokea. Na sasa mashabiki wake wananafasi ya kuweza kufarhia muziki wake.