Nimetimuliwa chuoni kufuatia mitikasi yangu mitandaoni - Brian Chira

Chira alisema kuwa anajivunia chochote anachofanya mitandaoni licha ya kuwa hiyo ndio ilikuwa sababu kuu ya kutimuliwa chuoni.

Muhtasari

• Chira alieleza kuwa chanzo kuu ni kuwa shule hiyo yenye misingi ya kikanisa ilihisi matendo yake mitandaoni ilienda kinyume na hili.

• Siku ya Jumatatu, Brian Chira alifikishwa mahakama ya Kibera baada ya kukamatwa siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa mitandaoni.

Brian Chira
Brian Chira
Image: Screengrab

TikToker maarufu Brian Chira amefichua kuwa amedai kufukuzwa kutoka chuo kikuu cha Kabarak kwa sababu makala yake kwenye mitandaoni iliyokuwa ikienda kinyume na kanuni za Chuo hicho.

Chira akizungumza kwenye mahojiano na Andrew Kibe baada ya kuachiliwa na mahakama ya Kibera kwa dhamana ya shilingi 50,000, alieleza kuwa chanzo kuu ni kuwa shule hiyo yenye misingi ya kikanisa ilihisi matendo yake mitandaoni ilienda kinyume na hili.

"Nimetimuliwa chuoni kwa sababu kulingana na chuo kikuu cha Kabarak ambayo motto yake ni elimu kwa misingi ya kikanisa na kwa hivyo walihisi kuwa vitendo vyangu mitandaoni haikuendanisha na motto yao."

Chira aliongeza kuwa alikamatwa na polisi alipokuwa chuoni baada ya kushtakiwa na muunda maudhui mwenza Azziad Nasenya kwa madai ya kumchfulia jina.

Siku ya Jumatatu, Brian Chira alifikishwa mahakama ya Kibera baada ya kukamatwa siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa mitandaoni na kuweza kutumia akaunti yake ya TikTok na kumtukana Azziad.

Kulingana na Getrude Kibare, wakili wa Azziad, live ya Chira kwenye mtandao wa Tiktok ilikuwa na matamshi ya kuudhi yaliyomlenga Azziad, yakitumia lugha mbaya na ya kudhalilisha.

Wakati huo huo, Chira alifichua bila kujali maelezo ya kibinafsi ya Azziad mtandaoni, na kumfanya apokee simu nyingi ambazo zinazomsumbua kutoka kwa watu asiowajua. jambo ambalo lilimsababishia dhiki kubwa.

Waunda maudhui ikiwa ni pamoja na Eric Omondi  na Oga Obinna walijitokeza na kumkashifu Chira kwa matusi aliyomtupia Azziad wengi wao wakisema ilikuwa muda mwafaka kwa watu wanatumia umaarufu wao kuwanyanyasa wenzao mitandaoni.