Mimi ndio msanii wa kwanza kutoa nyimbo 13 mfululizo na zote zikahit - Aslay

Msanii huyo alisema kwamba Bongo Fleva katika miaka 10 ambayo amehudumu amefanikiwa kuwalea wengin, akiwataja Marioo, Jay Melody kuwa baadhi ya wasanii waliopitia kwenye mikono yake.

Muhtasari

• Msanii huyo alizidi kusema kwamba anaona katika wasanii wengine wote, ni yeye tu anayeipiga jeki sana Bongo Fleva.

• Aslay alisisitza kwamba yeye ataishia tu katika muziki wa Bongo Fleva wala hatochanganya.

Aslay
Aslay
Image: Instagram

Msanii Aslay kwa mara nyingine tena amezungumzia wazo la kampeni ya miaka 10 kwenye muziki, kampeni ambayo ameipa jina ‘Mimi ni Bongo Fleva’.

Akizungumza katika runinga ya East Africa TV, Aslay anasema kwamba msukumo anaoupata kutokana na kujiita yeye ndio Bongo Fleva ni kwa sababu ndio muziki ambao umemlea kwa miaka kumi na ushee.

Msanii huyo ambaye awali alikiri bayana kwamba hadhani ipo siku ataketi chini na kuandika muziki wa Amapiano, alisema kwamba atakwama kwenye Bongo Fleva kwa vile yeye ndio kama anahisi msanii wa kwanza wa Bongo Fleva kuwahi kutokea ambaye alitoa nyimbo 13 kwa mfululizo n azote zikawa kubwa na kupata mapokezi ya kishujaa kutoka kwa mashabiki.

“Mimi naamini Bongo Fleva imenilea kuliko kitu kingine chochote, halafu mimi nahisi ni msanii wa kwanza kutoa nyimbo 13 mfululizo halafu zote zikafanya vizuri, Na zote ni Bongo Fleva, kwa hiyo naamini katika Bongo Fleva mimi ndio naeza nikawa mfalme,” Aslay alisema.

Msanii huyo alizidi kusema kwamba anaona katika wasanii wengine wote, ni yeye tu anayeipiga jeki sana Bongo Fleva, japo hakusita kuwatambua wengine amabo wanajitahidi kusimama na Bongo Fleva wakati huu ambapo wimbi la muziki wa Amapiano limeingia Zaidi.

“Naona wasanii wengine wnajitahidi lakini bado wanachanganya, lakini mimi bado sijachanganya, kwa hiyo naona kujipa jina hilo la Mimi ni Bongo Fleva sidhani kama ni vibaya,” Aslay alisema.

Msanii huyo alisema kwamba Bongo Fleva katika miaka 10 ambayo amehudumu amefanikiwa kuwalea wengin, akiwataja Marioo, Jay Melody kuwa baadhi ya wasanii waliopitia kwenye mikono yake.