William Ruto amekuwa crush wangu tangu kitambo akiwa MP - Sandra Dacha

Sandra Dacha alifichua kwamba uhusiano wake na Akuku Danger ulianza wakati walikutana katika mazishi ya mchekeshaji wa Churchill Show, Othuol Othuol.

Muhtasari

• "Zakayo amekuwa crush wangu kutoka kitambo hiyo lakini wakati mwingine nabadilisha mawazo yangu,” alisema.

Sandra Dacha.
Sandra Dacha.
Image: Facebook

Muigizaji Sandra Dacha amekiri kwamba rais William Ruto ndiye mtu mashuhuri ambaye ni crush wake.

Dacha alisema haya wakati wa mazungmzo na mchekeshaji Oga Obinna kwenye kipindi cha KulaCooler kwenye chaneli yake ya YouTube.

Mchekeshaji huyo ambaye hajawahi ona aibu kutokana na watu kuwadhihaki watu mitandaoni, alifunguka kwamba hajaanza kuwa na crush wa rais Ruto hivi majuzi bali ni kutoka kitambo kiongozi huyo alipokuwa mbunge wa Eldoret Kaskazini.

“Ruto, William. Naapa ni yeye. Tangu kitambo akiwa mbunge. Zakayo amekuwa crush wangu kutoka kitambo hiyo lakini wakati mwingine nabadilisha mawazo yangu,” alisema.

Obinna aliwambia kuchukua fursa hiyo kumuambia rais jambo moja, pengine atatazama kipindi hicho, akimsisitizia kwamba huenda hiyo ikawa ni fursa yake ya kuvuka mstari kutoka maisha ya kawaida kwenda maisha ya ukwasi.

“William Ruto kusema ukweli umekuwa crush wangu wa muda mrefu, tangu enzi zile ukiwa Mbunge,” alitoa neno kwa Ruto.

Kwa mara ya kwanza, muigizaji huyo ambaye pia ni mchekeshaji alisema kwamba mara ya kwanza walikutana na Akuku Danger ilikuwa ni katika mazishi ya mcheshi marehemu Othuol Othuol miaka michache iliyopita.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba anatarajia kumzalia Akuku mtoto pindi tu watakapofunga harusi.

Hata hivyo, uhusiano wake na Akuku, ambaye pia anasemekana kuwa na familia umekuwa ukichukuliwa kimzaha wengi wakihisi ni wa mitandaoni tu lakini katika uhalisia wa maisha ni marafiki tu.

Kwa upande wao, Sandra na Akuku wamekuwa wakisisitiza kwamba wao ni wapenzi na watafunga harusi hivi karibuni.

Sandra aliweka wazi kwamba yeye na Akuku ni mtu na mpenzi wake mwaka jana wakati alikuwa anaongoza kampeni ya kuchangisha pesa mitandaoni ili kugharamia matibabu ya Akuku Danger ambaye anaugua ugonjwa wa Seli Mundu.