Mshangao baada ya mwimbaji Nadia Mukami kukiri "Sijaolewa, bado niko soko!"

Arrow Bwoy ako nami kwa mkopo hadi atakapo nilipia mahari ndio nitakuwa mke wake rasmi. Mimi ni mpenzi wake tu si mke," Nadia alisema.

Muhtasari

• Msanii huyo alibainisha kuwa bado mchumba wake hakuwa amemlipia mahari kwa wazazi wake kwa hivyo haikuwa sawa kumtaja kama mke wa mtu.

• Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kuanzia mwaka wa 2021 na wezi huu watakuwa wakiadimisha mwaka wao wapili pamoja.

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAM

Malkia wa muziki wa Kenya Nadia Mukami, amewashtua Wakenya baada ya kukiri kuwa bado yupo soko (kuwa sokoni nikwa lugha ya mtaani ina maana kuwa hana mchumba) licha ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake, Arrow Bwoy kwa zaidi ya miaka miwili.

Wakati msanii huyo akizungumza na kituo kimoja cha radio cha humu nchini, alibainisha kuwa bado mchumba wake hajamlipia mahari kwa wazazi wake kwa hivyo sio sawa yeye kutajwa kama mke wa mtu.

"Mimi sijaolewa. Ukweli sijaolewa. Arrow Boy hata hajanilipa mahari kwa hivyo mimi bado niko soko. Ako namii kwa mkopo hadi atakapo nilipia mahari ndio nitakuwa mke wake rasmi. Mimi ni mpenzi wake tu si mke." Nadia alifichua.

Kulingana na mama huyo wa mtoto mmoja, wanaume walistahili kufahamu kuwa kama bado hawajawalipia wapenzi wao mahari, basi si sawa kuwataja wanawake walio kwenye mahusiano ya kimapenzi nao kuwa wake zao

Mnamo Agosti 2021, Nadia na Arrow Bwoy walithibitisha kuwa kwenye mahusiano baada ya kuwadokezea mashabiki wao mitandaoni kwa miezi kadhaa kuwa wanapendana.

Nadia pia alifichua kuwa anazeeka, na ilikuwa vyema kuwa na mpenzi.

"Nadhani watu hawaamini kwa sababu kwa muda mrefu zaidi. Nimeanza kuzeeka, nina miaka 25 mwaka huu, na inafikia umri fulani unataka kujivunia mtu na kujenga maisha ya baadaye naye," alisema miaka miwili iliyopita.

Kulingana na wapenzi hao, hatua ya mazungumzo ya uhusiano wao ilianza wakati wa kutengeneza wimbo wao maarufu, Radio Love.

"Sikupenda wimbo huo kwa sababu kuna wakati tungeenda kutumbuiza huku tukiwa tumekosana. Unapoimba na mpenzi wako, ikiwa mmekosana kidogo inakuwa viguu kutumbuiza na shabiki hawatafurahia kazi yenu," Nadia Mukami alikiri.

Arrow Bwoy alifichua kwamba alimpenda Nadia kabla ya kufanya kolabo ya Radio Love.

"Nilikuwa nimekuona kama msanii mzuri ambaye ana mahusiano mazuri na kila mtu, kisha tukazungumza kuhusu collabo. Wakati wa kurekodi wimbo huo, nilikuwa mgonjwa. Lakini ilibidi nirekodi muziki huo kwa sababu ya msanii huyu wa kike anayefanya kazi kwa bidii," alisema Arrow Bwoy.