logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wasanii wananunua watazamaji wa YouTube- Zuchu alalamika

"Nawaza sana kama msanii, umejisikiaje kununua viewers? Ni kama unakuwa unajua nafasi yako ila ndiyo hivyo tena unaificha ficha kimoyomoyo," Zuchu aliwaza.

image
na

Habari04 August 2023 - 10:45

Muhtasari


• Zuchu amelalamikia namna baadhi ya wasanii wenzake kutoka Tanzania wamezamia katika kununua watu wa tutazama muziki wao katika mitandao kama YouTube.

Msanii Zuchu

Msanii wa nyimbo za bongo fleva Bi. Zuhura Othman almaarafu Zuchu amelalamikia namna baadhi ya wasanii wenzake kutoka Tanzania wamezamia katika kununua watu wa tutazama muziki wao katika mitandao kama YouTube.

Mwimbaji huyo ambaye wimbo wake wa Sukari ulivuma sana, anadai kuwa wanamuziki katika taifa hilo, wengi wao hawaziimbi nyimbo ambazo zinaweza kuvuma kama zake, ila badala yake wanawalipa watu ili nyimbo hizo ziweze kutazamwa.

Katika ukurasa wake wa Instragram, Zuchu aliposti akielekeza lawama na shutuma hizo kwao, akidai kuwa hata baadhi wanafanya hivyo kisiri." Nawaza sana kama msanii, umejisikiaje kununua viewers? Ni kama unakuwa unajua nafasi yako ila ndiyo hivyo tena unaificha ficha kimoyomoyo...unajisikiaje kwani. Ni Tanzania pekee." Aliposti kwa mnuno.

Msanii huyo wa WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz tayari ameutoa wimbo wake mpya unaofahamika kama Honey, na ambao kwa kipindi cha siku saba wimbo huo umeweza kutazamwa na watazamaji milioni 2.4.

Katika utafiti uliofanya mwezi Juni na Charts Tanzania, msanii huyo aliorodheshwa nambari tatu, na wa kwanza wa kike, akiwa miongoni mwa wasanii ambao nyimbo zao zilitazamwa sana kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Aidha, Zuchu tangu ajiunge na shirika la kurekodi nyimbo la Wasafi, na ambalo mmiliki anadaiwa kuwa mpenziwe, amekuwa akivuma sana katika shoo zake ambazo huzifanya katika Afrika mashariki na pia kimataifa.

Tangu alipojiunga na shirika hilo 2020, mwimbaji huyo tayari ametoa nyibo saba, ambazo zimevuma sana katika kanda ya Afrika Mashariki, tangu aliposhirikishwa na Rayvanny katika wimbo wa Number One.

Baadhi ya nyimbo zingine zilizovuma sana ni pamoja na Sukari, Nitalia Kwikwikwi, Nani na nyinginezo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved